Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati akifungua rasmi Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 na Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Na Mwandishi wetu – Malunde Media
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka Wanawake nchini Tanzania kujiamini na kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao kwani Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameudhihirishia Ulimwengu kuwa Wanawake wanaweza kuwa viongozi.
Mhe. Senyamule ametoa kauli hiyo Agosti 27, 2024 wakati akifungua rasmi Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 na Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
“Safari hii wanawake wote tujitokeze kugombea nafasi za uongozi kwa sababu yupo Mwanamke (Mhe. Rais Samia) aliyeonesha kuwa wanawake tunaweza. Ni imani yangu katika uchaguzi wanawake wengi watawania nafasi za uongozi kwa sababu jamii imejionea kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, jamii imeamini kuwa wanawake wanaweza na mfano hai ni Mhe. Rais Samia”, amesema Mhe. Senyamule.
“Ili usawa wa kijinsia ufikiwe ni lazima wanawake tuchukue hatua, mazingira rafiki yamewekwa hivyo ni kazi kwetu kupambana. Ni lazima tuchukue hatua za kugombea na kuingia katika ngazi za maamuzi”,ameongeza Mhe. Senyamule.
Aidha amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kufanya jitihada mbalimbali kutekeleza mpango kazi wa Beijing kufikia usawa wa kijinsia ambapo sasa wanawake wengi wameshika nafasi za uongozi na Rais Mhe. Samia Suluhu ameendelea kufanya teuzi mbalimbali kwa wanawake wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na taasisi mbalimbali.
“Tunaposherekea miaka 30 ya Beijing tunayo mengi ya kujivunia. Nafasi za wanawake katika uongozi zinazidi kuongezeka, tunaendelea kuboresha huduma za afya, elimu, upatikanaji wa maji safi na salama, umeme na ongezeko la madawati ya jinsia”,ameeeleza.
Katika hatua nyingine ameitaka jamii kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia akibainisha kuwa mauaji yanayoongoza katika Mkoa wa Dodoma yanasababishwa na ulevi na wivu wa mapenzi.
“Tuweke nguvu kuelimisha jamii watu wasifanye ukatili, asilimia kubwa ya matukio ya ukatili yanafanyika majumbani na jamii inaficha taarifa za matukio, tusitumie nguvu kubwa kutetea wahalifu, tutoe maonyo na elimu kabla ya ukatili haujafanyika..Na lazima tuchukue hatua ya kuwafundisha watoto maadili mema”,ameongeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amesema suala la usawa wa kijinsia ni suala la maendeleo hivyo amewahamasisha wananchi kutoa maoni kwenye dira ya Taifa 2050 kwa ajili ya mwelekeo wa taifa kwa miaka 25 ijayo kwa kuzingatia haki na usawa wa Kijinsia katika masuala yote ya maendeleo.
Liundi amesema nchi ya Tanzania imepiga hatua katika masuala ya usawa wa kijinsia ambapo sasa wanawake wanashika nafasi za uongozi akitolea mfano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.
“Tunatambua kuwa kwa sasa nchi yetu ina Rais Mwanamke kwa mara ya kwanza kabisa; kwa upande wa wabunge wanawake ni asilimia 37 tu ambao 9.5% ni wabunge wa kuchaguliwa na 29% ni wa vitimaalumu. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ni miongozi mwa wanawake wakuu mikoa wachache nchini na pia, mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa ni miongoni mwa wakuu wa wilaya wanawake wachache nchini”, amesema Liundi.
Tamasha hilo la siku tatu (Agosti 27 – 29 , 2024 linaloongozwa na mada kuu ‘Dira Jumuishi ya 2050: Miaka 30 Baada ya Beijing Tujipange’ linashirikisha Wanaharakati na Wadau zaidi ya 300 wanaotetea haki za wanawake na usawa wa jinsia kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali amesema Tamasha la Jinsia ni moja ya majukwaa ya TGNP katika ujenzi wa nguvu za pamoja ambapo Jukwaa hilo ni la wazi kwa ajili ya wanawake na wadau wa haki za binadamu ambao hukutana pamoja kila baada ya mwaka mmoja kubadilishana uzoefu, kusherehekea, kutathmini na kupanga mipango ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Akilimali amewasisitiza wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuepuka kuwa wapiga makofi na wasindikizaji wa wanaume kwenye uchaguzi.
“Wanawake tuwajibike, tujitokeze kugombea nafasi za uongozi badala ya kubaki kuwa walalamikaji na wapiga makofi tu”,amesema.
Amesema ili kufikia mikakati juu ya matumizi ya nishati safi ameihamasisha Serikali kupunguza gharama za gesi na tozo za gesi ili kuwawezesha wananchi walipo vijijini na wengi kutumia nishati safi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati akifungua rasmi Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 na Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali Agosti 27, 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma. Picha na Malunde Media
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati akifungua rasmi Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 na Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati akifungua rasmi Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 na Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati akifungua rasmi Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 na Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 7 la Jinsia Ngazi ya Wilaya 2024 katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akikata utepe ishara ya kufungua Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akikata utepe ishara ya kufungua Maonesho ya Shughuli za Wajasiriamali katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (wa pili kushoto) akipata maelezo kwenye banda la TGNP katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akisoma Ilani ya Madai ya wanawake katika uchaguzi (Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake – Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025) yenye lengo la kudai mabadiliko ya mifumo kandamizi inayohalalisha ubaguzi wa wanawake katika uchaguzi kama wapiga kura, wenye kuwania nafasi za teuzi na hatimaye kuwakwamisha kwenye kuchaguliwa kama wawakilishi katika ngazi mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akisoma Ilani ya Madai ya wanawake katika uchaguzi (Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake – Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025)