SABABU YA KUCHELEWA KUANZA KWA VAR TANZANIA HII HAPA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi ameweka wazi sababu inayosababisha kuchelewa kutumika kwa Video Assistas Refferee (VAR) katika ligi kuu Tanzania Bara. Kasongo amesema, wamepokea taarifa kutoka CAF kwamba lazima waamuzi wapate walau session tano za mafunzo kuhusu matumizi ya VAR.

 

 

 

 

Hii inatokana na kuwa Tanzania haina mwamuzi hata mmoja ambaye amefuzu katika mafunzo ya matumizi ya VAR.

 

 

“Mpaka sasa kinachochelewesha ni mafunzo ya waamuzi, maana Tanzania haitoi waamuzi katika mashindano makubwa yanayohusisha VAR, hivyo CAF walituelekeza kutoa mafunzo kwa waamuzi wetu kwanza kabla ya kutumia” – Almasi Kasongo.

 

 

Almasi Kasongo pia ameweka wazi kuwa mafunzo hayo ya waamuzi yatasaidia kupunguza gharama ambayo ingeongezeka ya kuchukua waamuzi kotoka nje ya nchi kwa ajili ya kuendesha VAR endapo tungetaka kutumia VAR.

Related Posts