TAARIFA mbaya kwa beki mpya wa Simba, Valentin Nouma ni kwamba kocha Brama Traore, amemtema katika kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso, huku Stephanie Aziz KI wa Yanga akiendelea kupeta.
Nouma amekutana na taarifa hiyo ya kushtua ikiwa ni mara ya kwanza tangu atue Simba iliyomsajili dirisha kubwa la usajili lililopita, huku akiwa hajawahi kuanza katika kikosi hicho cha Wekundu kwenye mechi mbili za Ligi, kwani Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliendelea kuishikilia nafasi hiyo kwa sasa.
Wakati Nouma, aliyekuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Burkina Faso katika fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 iliyofanyika mapema mwaka huu huko Ivory Coast akitemwa, nyota wa Yanga, Azizi KI ameendelea kuaminiwa akiwa ndani ya orodha ya wachezaji 25 walioitwa kambini.
Burkina Faso inayojiandaa na mechi za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika 2025, ikicheza dhidi ya Malawi na Senegal imewajumisha wachezaji watano tu wanaocheza soka Afrika.
Kwenye orodha hiyo wapo makipa, Herve Koffi (RC Lens, Ubelgiji), Killian Nikiema (ADO Den Haag, Uholanzi) na Farid Ouedraogo (Vita Club, DR Congo).
Mabeki ni; Edmond Tapsoba(Bayer Leverkusen, Ujerumani), Steeve Yago(Aris Limassol, Cyprus), Yacouba Djiga (Etoile Rouge de Belgrade, Serbia), Adamo Nagalo (FC Nordsjælland, Denmark), Issa Kabore(Manchester City, England), Mohammed Ouedraogo(SCR Altach, Austria), Trova Boni (San Antonio FC, USA) na Mohammed Yabre(ASEC Mimosas,Ivory Coast).
Viungo ni; Gustavo Sangare (FC Noah, Armenia), Ibrahim Toure (Pyramids, Misri), Cedric Badolo (Sheriff Tiraspol, Moldova), Sacha Banse (Greuther Fürth, Ujerumani), Saidou Simpore (National Bank, Ujerumani), Dramane Salou (Hapoel Haifa, Israel), Azizi KI (Yanga, Tanzania).
Wapo washambuliaji saba ambao ni; Dango Ouattara (FC Bournemouth, England), Ousseni Bouda (San Jose Earthquakes, USA), Lassina Traore (FC Shakhtar Donetsk, Ukraine), Bureima Bande(Veikkausliiga, Sweden), Mohammed Konate (Al Riyadh, Saudi Arabia), Abdul Ouattara (Episkopi, Ugiriki) na Ousmane Camara (Angers, Ufaransa).