BAOBAB WATEMBELEA NBAA – MICHUZI BLOG

BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa elimu/mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za Sekondari ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli mbalimbali za Bodi na kukuza taaluma ya Uhasibu.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Huduma za Shirika CPA Kulwa Malendeja alitoa salamu kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno ambaye alitamani kuwepo kwenye mafunzo hayo lakini kutokana na majukumu mengine ameshindwa.

Pia amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kuwa Mhasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi.

Aliongeza kuwa wanafunzi wa Kozi nyingine ambazo hazihusiani na masomo ya Uhasibu nao wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na wataanzia masomo ya ngazi ya kwanza (foundation level) tofauti na wale waliosomea masomo ya Uhasibu na pia waliomaliza kidato cha nne na sita na wanacheti wanaweza kufanya mitihani ya Bodi alisema Malendeja.

Akiishukuru NBAA, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Baobab Stephen Gervas Mahundi amesema Bodi kwa mwaliko wa wanafunzi ili kuja kupata Elimu ya Uhasibu.

Aliongeza kuwa wanafunzi waliotembelea Bodi ni  wanafunzi wa kidato cha tano wa wanaosoma masomo ya biashara katika shule hiyo ambao itawapa dira na mwelekeo mzuri sasa na hapo baadae.

Mkurugenzi wa Huduma za Shirika CPA Kulwa Malendeja akizungumza kwa  kuwakaribisha pamoja na kufungua mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea NBAA.

Baadhi ya watumishi wa NBAA wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya walimu pamoja na wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab.

Related Posts