Dr Ndumbaro atilia mkazo uwanja wa Arusha utakamilika kwa wakati

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesisitiza kuwa ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa miguu wa Arusha utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na kuwa tayari kwa michuano ya AFCON 2027.

Akizungumza katika ziara ya kukagua maendeleo ya uwanja huo leo Agosti 29, 2024 Mhe.Ndumbaro amewahakikishia Watanzania kuwa ujenzi wa uwanja huo utakamilika kwa wakati kutokana na kasi na uwezo wa mkandarasi anayetekeleza ujenzi huo.

Amewataka wananchi wa Jiji la Arusha na maeneo mengine waendelee kutoa ushirikiano kwa Serikali ili maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza, kuendeleza na kukuza fursa za ajira kwa Watanzania kupitia sekta ya michezo yaweze kutimia kupitia mradi huo.

Ujenzi wa uwanja huo katika hatua ya awali umefikia 5% ikihusisha uandaaji wa eneo la uwanja, manunuzi na ujenzi wa ofisi za mkandarasi.

Related Posts