JOHN Bocco staa wa zamani wa Simba, juzi alishuka uwanjani kwa mara ya kwanza msimu huu ikiwa ni wa 17 kwake tangu 2008 akiwa na JKT iliyolazimishwa suluhu na Azam FC.
Alicheza ligi mara kwa mwisho Desemba 23 mwaka jana wakati akiichezea Simba dhidi ya Kagera Sugar.
Kitendo cha kukaa nje kwa muda mrefu bila kucheza, wengi wao waliamini pengine katundiga daluga, alilifafanua hilo; “Sio Simba wala mimi, sikuwahi kutangaza kama nastaafu, Simba ilinipa majukumu ya kukinoa kikosi cha vijana kwa sababu nilisomea ukocha.”
Lakini baada ya kutoitwa Taifa Stars kwa muda wa mwaka mmoja, John Bocco ‘Adebayor’ ametoa ya moyoni. Ametangaza kutundika daruga rasmi kuitumikia timu hiyo ya taifa, huku akiweka bayana kwa klabu hana muda mrefu kabla ya kustaafu na kujikita katika ukocha.
Nyota huyo wa zamani wa Cosmopolitan, Azam na Simba, alianza kuitumikia Stars tangu mwaka 2009 na mara ya mwisho kuitwa na kucheza ilikuwa Septemba 7 mwaka jana wakati Stars ilipoumana na Algeria katika mechi ya kuwania fainali za Afcon zilizopita na mchezo huo kuisha kwa suluhu jijini Algers.
Alisema ameamua kustaafu kuichezea timu hiyo na kwa sasa anamalizia soka lake ngazi ya klabu ambapo pia hana muda mrefu kabla ya kuachia ngaziĀ muda si mrefu.
Bocco aliyeitumikia timu hiyo katika mechi 84 akishika nafasi ya tano ya waliocheza mara nyingi nyuma ya Erasto Nyoni (107), Mrisho Ngassa (100), Kelvin Yondani (97) na Simon Msuva (92), huku akiifungia mabao 16 akishika nafasi ya nne nyuma ya Ngassa (24), Msuva na Mbwana Samatta (22).
Bocco alitoa msimamo huo wa kuivua jezi ya Stars baada ya kuulizwa bado anaiona nafasi ya kuitumikia Stars wakati huu akiwa JKT Tanzania.
“Hapana siwezi tena kurejea kikosini, ni wakati wa wengine kulitumikia taifa,” alijibu Bocco anayeshikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 154 katika misimu 16 akimpiku Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ aliyefunga mabao 153 katika misimu 13.
Bocco alishuka uwanjani kwa mara ya kwanza msimu huu ikiwa ni wa 17 kwake tangu 2008 akiwa na JKT iliyolazimishwa suluhu na Azam FC, ikiwa ni baara ya kucheza mara kwa mwisho Desemba 23 mwaka jana wakati akiichezea Simba dhidi ya Kagera Sugar.
Kitendo cha kukaa nje kwa muda mrefu bila kucheza, wengi wao waliamini pengine katundiga daluga, alilifafanua hilo; “Sio Simba wala mimi, sikuwahi kutangaza kama nastaafu, Simba ilinipa majukumu ya kukinoa kikosi cha vijana kwa sababu nilisomea ukocha.”
“Tanzania haijazoeleka kuona mchezaji anacheza na kusomea ukocha, nilianza kusoma muda kwa sababu nina malengo ya kuwa kocha mkubwa. Kuhusu kustaafu kucheza Ligi Kuu nina muda mfupi, ingawa sijui lini nitastaafu, nikiwa tayari Watanzania watajua,” alifafanua mshambuliaji huyo mkongwe.
Mbali na hilo, alizungumzia kuhusiana na JKT, akisema wamejipanga kuhakikisha wanafanya vitu vikubwa ili kutimiza malengo ya timu.
“Niwaambie mashabiki waendelee kutuunga mkono, ili tuwe na umoja kuweza kutimiza malengo yetu, nashukuru kwa ushirikiano wao wanaonionyesha,” alisema Bocco aliyemaliza msimu uliopita akiwa na mabao matatu akiwa anashikilia rekodi ya kufunga misimu 16 mfululizo akiwa na Azam na Simba.