Kazi ipo eneo la kushuka daraja BDL

WAKATI Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) ikizidi kushika kasi, mchuano umehamia kwa  timu zitakazoshuka daraja kazi ikiwa kwa timu tano zinazochuana zisishuke.

Timu hizo ni KIUT yenye pointi 30, Jogoo (28), Ukonga Kings (27), Crowns (27) na Chui (25), zipo katika mtihani huku tatu kati ya hizo ndizo zitakazoshuka daraja.

Zitakazoshuka daraja zitajulikana pale kila timu zikishacheza michezo 30.

Wakati timu hizo zikichuana katika vita ya kushuka daraja, timu zilizopo katika nafasi ya kucheza hatua ya nane bora ni Dar City yenye pointi (48), UDSM Outsiders (48), Savio (45),  na JKT (42).

Nyingine ni Mchenga Star yenye pointi 40, Vijana ‘City Bulls’ (39), ABC (38), Srelio (36), DB Oratory (35), Pazi (32) na Mgulani  JKT (31) kati ya hizo zitaungana na  timu nne za juu.

DB Troncatti yaendelea kukimbiza

IKIWA zimesalia michezo minne kwa baadhi ya timu kabla ya kumalizika kwa duru la pili la Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), DB Troncatti inaendelea kuongoza kwa upande wa Wanawake ikiwa na pointi 49 katika msimamo wa ligi hiyo.

Timu inayoifukuzia kwa karibu ni Pazi Queens iliyopo nafasi ya pili ikiwa na pointi 45, huku  Tausi  Royals ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 44.

Vijana Queens (43), Jeshi Stars (41), DB Lioness (41), JKT Stars (40),Polisi Stars (38) na Mchenga Stars (35).

 Zingine ni City Queens (34),Ukonga Queens (32), Mgulani Stars (30), Twalipo Queens (29), UDSM Queens (28), Kigamboni Queens (27) na Kurasini Divas (23).

TIMU                     PL    W    L     PTS

DB Troncatti        26     3     3     49

Pazi Queens         26    19   7      45

Tausi Royals         24    20   4     44

Vijana Quees        23     20   3     43  

Jeshi Stars             23     18   5      41

DB Lioness            25     16   9     41

JKT Stars                21    19    2     40

Polisi Stars             25    13   12   38

Mchenga Queens 25     10   15  35

City Queens           25     9     16  34

Ukonga Queens     25     7     18  32

Mgulani Stars        22      8     14   30

Twalipo Queens     24    5     19     29

UDSM Queens        26    2      24    28

Kigamboni Queens    25    7   18   27

Kurasini Divas             22     3   17   23 

Related Posts