Mwenezi Makalla akagua ujenzi wa hospital ya mbagala,ujenzi wa shule Mangaya asisitiza miradi ikamilike kwa wakati.

Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla leo akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kukagua na kuzungumza na Wananchi wa Majimbo 10 ya Mkoa wa Dar es salam na leo ni Jimbo la Mbagala amekagua ujenzi wa hospital ya Mbagala yenye hadhi ya Hospital ya Wilaya na ujenzi wa shule ya ghorofa Sekondari ya Mangaya Mbagala .

Mwenezi Makalla amesema “Ujenzi huu Hospital ya Mbagala naujua tangu nikiwa RC Dar es salam na nilipambania sana ujenzi wake , Ujenzi huu utapunguza msongamano wa Wagonjwa katika hospital ya wilaya ya Temeke lakini kuokoa muda kwa Watu Jimbo la Mbagala ambao wanaotoka mbali hivyo tumshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kuendeleza adhma yake ya kuipambania sekta ya Afya na ujenzi huu unaogharimu bilioni 10 tayari bilioni 04 zimeletwa na serikali kuu.

Upande wa shule ya sekondari ya ghorofa ya Mangaya Mwenezi Makalla amesema kwa Ujenzi huu ni heshima kwa wana Mbagala kikubwa miradi hii muitunze kwani Dkt Samia Suluhu Hassan ameamua kufanya makubwa sekta ya elimu kubwa mhakikishe miradi hii mnaikamilisha kwa wakati.

Related Posts