Msaanii Mbosso kutokea katika record lebal ya WCB amewasilia katika viunga vya manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera na kupitishwa katika maeneo tofauti tofauti ya Manispaa ya Bukoba huku akishare love na mashabiki zake waliojitokeza kwa wingi kumpokea huku wengine wakimsubilia barabarani.
Mbosso amewasili Mkoani Kagera kwa ajili ya Show kubwa ya Muleba Festival inayotarajia kufanyika August 31 siku ya Jumamosi katika viwanja vya Zimbihile vilivyopo katika Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera huku akitarajia kuwa sambamba na wasanii wengine wakali kutokea Dar Es Salaam akiwemo Chino wanaman ,Dula Makabila,wazee wa makoti yaani Missomisondo,Juma Nature pamoja na wengine kutoka hadi nje ya Nchi akiwemo John Blaq kutokea Nchini Uganda
Haya yote yamefanyika chini ya waandaaji ambao ni Magical Lounge na wameleta burudani hii Mkoani Kagera kwa ajili ya kuwafurahisha wakazi wa maeneo haya ikiwa ni sambamba na kuwapa fursa za kiuchumi, Ayo Tv tulikuwepo katika eneo la tukio kukuonyesha yaliyotokea katika mapokezi hayo ikiwa ni kuelekea show ya Jumamosi ya tarehe 31 ambapo pia tutakuletea updates mbalimbali kupitia katika page zetu.
The post VIDEO:Balaa la Mboso alivyopokelewa Bukoba,mashabiki washindwa kujizuia first appeared on Millard Ayo.