Dar es Salaam. Mkazi wa Mvumoni jijini hapa Ramadhan Utulo(38), amefikishwa katika mahakama ya Wilaya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kubaka mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 12.
Utulo alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka na Wakili wa Serikali Harrison Lukosi mbele ya Hakimu Irene Josiah.
Lukosi alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya Julai Mosi hadi Agosti 19, 2024, maeneo ya Mvumoni Wilaya ya Kinondoni alimbaka mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi naye na mama yake pamoja na watoto wengine.
Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa Jamhuri ulidai upelelezi umekamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe ya kumsomewa maelezo ya awali.
Hakimu Irene alisema shauri hilo linadhaminika kwa mujibu wa sheria na amemtaka mshtakiwa huyo awe na wadhamini wawili wenye barua zinazotambulika watakaosaini bondi ya Sh1 milioni.
Mshitakiwa amekidhi masharti ya na sasa yupo nje kwa dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi shauri liliahirishwa Septemba 9, 2024.