Jinsi mawakili wa kina Magoma, Yanga walivyochuana

Akifafanua hoja ya kwanza, wakili Rashid  (wa Yanga) amedai kuwa uamuzi ambao kina Magoma wameukatia rufaa ni uamuzi mdogo ambao kwa mujibu kifungu cha 74 (2) cha Sheria ya Mashauri ya Madai (CPC), Sura 33, haukatiwi rufaa.

Huku akirejea uamuzi wa kesi moja iliyowahi kuamuriwa na aliyekuwa Jaji Mkuu, Francis Nyalali, Wakili Rashid  kwa kuwa hauamui haki za msingi za wadaawa na wala hauhitimishi shauri la msingi, bali hudumisha hali iliyopo kusubiri uamuzi wa shauri la msingi.

Amedai kuwa haki za msingi za wadaawa ziliamuriwa katka shauri la marejeo ambapo warufani walikuwepo wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo na waliwakilishwa ma nawakili wao.

Kuhusu hoja ya pili, wakili Rashid amefafanua kuwa rufaa hiyo imeshapitwa na wakati kwa kuwa tukio linatokana na uamuzi wanaoukatia rufaa (shauri la maombi ya marejeo) lilishapita, kwani shauri hilo la marejeo tayari lilishatolewa uamuzi, hivyo hakuna kinachoweza kubadilishwa.

Amesema kuwa nafuu za msingi walizoziomba Mahakama ya Kisutu ilisikilizwa mbele ya warufani pamoja na mawakili wao.

Ameongeza kuwa na uamuzi wa shauri la marejeo walilolifungua namba 17939/2024 kati ya Bodi ya Wadhamini wa Yanga dhidi ya Juma Ally na Mwaipopo na Abeid Abeid baada ya kuruhusiwa ulitolewa Agosti 9, 2024 Katika shauwi la maombi namba.

“Mheshimiwa Jaji kwa mujibu wa hoja hizo ni maombi ya mrufaniwa wa kwanza (Bodi ya Wadhamini wa Yanga) kwamba rufaa hii iitupilie mbali kwa gharama”, amesema wakili Rashid.

Akijibu hoja hizo, Wakili Mashenene amepinga pingamizi hilo huku akitoa maana ya uamuzi au amri ambazo hazipaswi kukatiwa rufaa (interlocutory orders) kwa kuirejesha mahakama hiyo katika uamuzi wa Mahakama ya Rufani kwenye kesi ya Seif Sharif Hamad dhidi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Amesema kuwa huo ni uamuzi au amri ambayo inahusiana na shauri masuala yanayohusiana na shauri husika lakini haitoi hitimisho la shauri hilo.

Wakili Mashenene pia akirejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika mashauri mbalimbali amesema kuwa mahakama hiyo imeweka vigezo vya kupima kama uamuzi au amri hiyo ndogo, akibainisha kuwa ni pamoja na aina ya nafuu zinazotokana na amri hizo, kama hazihitimishi shauri.

Amesema kuwa katika kumbukumbu za Mahakama ya Kisutu  shauri la Yanga la kuongezewa muda lilikuwa ni shauri linalojitegemea na kwamba nafuu zilizoombwa ni pamoja na kuongezewa muda kufungua shauri la marejeo.

Hivyo amedai kuwa uamuzi wa nafuu hizo ulihitimisha kabisa shauri hilo hapakuwa na shauri lingine mahakamani lililouwa linasubiriwa kusikilizwa (kabla ya Yanga kufungua shauri la marejeo)

Kuhusu hoja ya pili amedai kuwa si tu kwamba haina msingi lakini pia haifai kuwa pingamizi la awali kwa sababu, haikidhi matakwa ya kisheria ambayo yanataka hoja hiyo iwe ni ya kisheria na si ya kiushahidi.

Amesisitiza kuwa kwa kuzingatia hoja hizo hoja ya pili haifai kuwa pingamizi la awali kwa kuwa inahitaji Mahakama kuchunguza kama uamuzi huo unaolalamikiwa hauna athari kwa—-na kama ulitokana na shauri la msingi na kwamba hilo linaweza kuamuriwa wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo.

“Hivyo, kwa kuzingatia mawasilisho hayo tunaomba mahakama hii iitupilie mbali hoja zote za pingamizii na kwa gharama”, amesema wakili Mashenene.

Lakini wakili Rashid naye amepinga hoja za wakili Mashenene huku akidai kuwa katika baadhi ya hoja ametoa tafsiri isiyo sahihi akirejea muktadha wa uamuzi wa kesi ya Seif Sharif Hamad na SMZ.

Badala yake alifafanua uamuzi wa kesi hiyo akisisitiza kuwa unaakisi hoja zake katika hoaj zinazobishaniwa

Kwa hiyo mahakama inapaswa kuzingatia matokeo ya mwisho ya uamuzi unaokatiwa rufaa Katika kuamua.kama ni Interlocutory, na sisi tunasema ndio.

Related Posts