WANANCHI WAAHIDI KULINDA BWAWA LA MINDU – MWANAHARAKATI MZALENDO

Wananchi wa Kijiji cha Tangeni Kata ya Mzumbe Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero wameahidi kulinda na kulihifadhi Bwawa la Mindu linalotegemewa na wakazi wa Manispaa ya Morogoro kwa zaidi ya asilimia 75 ya upatikanaji wa Majisafi na Salama.

Hayo yamebainishwa leo na wananchi hao baada ya wataalamu kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Morogoro (MORUWASA) kufika katika Kijiji hicho kwa lengo la kuutambulisha Mradi wa Uhifadhi wa Bwawa la Mindu unaotekelezwa kuoitia Ufadhili wa Shirika la World WaterNet wenye lengo la kuhifadhi mazingira ya eneo la Bwawa la Mindu kupitia Kilimo Msitu.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi kwa wananchi Bi. Mishy Salim Kombo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Jumuiya za Watumia Maji kutoka Wami/Ruvu amesema Mradi huu ni Shirikishi hivyo Bodi itaendelea kuwashirikisha wananchi katika maeno yote yenye vyanzo vya maji ili kuleta dhana ya pamoja ya utunzaji wa Rasilimali hiyo.

Mbali na hilo, wakazi wa kijiji hicho cha Tangeni wameeleza namna walivyofurahishwa na mradi huo na kusema kuwa wapo tayari kupanda miti na kufanya kilimo msitu ili kunusuru mito yote inayotiririsha maji katika Bwawa la Mindu.

“Tone la maji lazima lihifadhiwe “

Related Posts