KIMEI ACHANGIA SHILINGI MILIONI TANO UJENZI WA MADRASA MSIKITI MKUU WA TAQWA – BAKWATA KAHE

NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo Dkt Charles Stephen Kimei ameendelea kuunga mkono juhudi za madhehebu ya dini katika kujenga miundombinu mbalimbali yenye lengo la kutoa huduma za kiimani na kujenga maadili kwa jamii.

Katika kuhakikisha hilo ametekeleza ahadi yake ya shilingi milioni tano yenye lengo la kuwaunga mkono waumini wa imani ya kiislamu msikiti mkuu wa Taqwa Bakwata kata ya Kahe walioamua kujenga vyumba viwili vya elimu ya awali pamoja madrasa kwa kujitolea wao wenyewe kwa hali na mali pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali.

Uongozi wa msikiti huo pamoja na BAKWATA kata ya Kahe wamemshukuru Dkt Kimei na kumpongeza kwa kutowabagua wananchi anaowawakilisha kwa imani zao.

Dkt Kimei amewaomba viongozi wote wa dini kuendelea kuiombea Tanzania na kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuiongoza Nchi katika usawa na haki.


Related Posts