Mh.Sillo awajulia hali majeruhi wa ajali mkoani Manyara

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Daniel Sillo amesema Serikali itaendelea kuwachukulia hatua za Kisheria madereva wote wasiotii na wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

 

Mhe Sillo amezungumza hayo leo Agosti 31,2024 alipofika kuwajulia hali wanafunzi 30 wa shule ya sekondari Endasaki waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara baada ya kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari mawili kati ya Scania na Coaster katika kijiji cha Gajal wilaya ya Babati.

 

Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wanne wanafunzi watatu wa kike na dereva aliyekuwa akiwaendesha.

Related Posts