Tanzania yajiweka mahala pazuri katika utekelezaji wa mkataba IOMOU

TASAC yaweka mikakati katika usimamizi wa utekelezaji wa mkataba kwenda katika uchumi wa Bluu

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 

Imeelezwa kuwa Tanzania imeweza kutekeleza hati ya makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi (IOMOU) katika kufanya ukaguzi wa Meli za Kigeni na kuwa mfano wa kuigwa.

Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu ,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Haji Makame wakati akifunga mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano  ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi (IOMOU) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema tangu kuingia kwa makubaliano hayo Tanzania imefikisha miaka 25 na kuwa na matokeo chanya kutokana jitihada za Serikali kutoa mafunzo mbalimbali ya Wakaguzi wa Meli Ndani na Nje ya Nchi  na kuweza kukagua vyombo vya majini 300.

Makame amesema ziko Jumuhiya Sita ambazo ziko nje ya Bahari ya Hindi ambao wameshiriki  mkutano  wa 27 wa Kamati ya kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi na kujionea hatua nzuri ya namna  mkataba  kwa nchi wanachama wa unavyotekelezwa.

Amesema kuwa kuna utaratibu wa kubadilishana taarifa za vyombo vinavyotoka Tanzania vikionekana katika nchi wanachama wanatoa taarifa kuhusiana na masuala ya ukaguzi.

Aidha amesema  miaka 25 nchi imekuwa katika mkakati wa  kuhakikisha vyombo vya usafiri majini vinakuwa salama. 

Amesema kadri nchi inavyofanya vizuri ndio inafanya kuwepo matokeo mazuri kutokana na vigezo vilivyowekwa na nchi wanachama.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Nahson Sigalla amesema ni mkutano maalum  umeshirikisha nchi wananchama Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli za Kigeni katika ukanda wa Bahari ya Hindi ukiwa lengo ya kuimarisha usalama katika vyombo.

Amesema kuimarisha usalama ni kulinda mazingira na matokeo yake kupata maendeleo endelevu ya kiuchumi.

Amesema  Tanzania imekuwa mfano katika ukaguzi wa Meli kutokana mafunzo  kwa wakaguzi kutokana na Meli zilizopo ni za kisasa.

Sigalla amesema wamekubaliana Kila nchi wanachama kufanya ukaguzi wa Meli za Kigeni angalau asilimia 10 ili kuweza kuwa na usalama wa kufanya nchi wananchama ziendelee kupata maendeleo. 

Amesema kuwa katika kufanya ukaguzi na kulinda mazungira ndio nguzo katika kwenda katika uchumi wa Bluu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Haji Makame akizungumza wakati akifunga Mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi (IOMOU) wenye lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya ukaguzi meli zinazoingia katika bandari za nchi wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Usalama wa Usafiri na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi Stella Katondo akitoa maelezo kuhusiana na Mikakati ya usimamizi wakati kufunga Mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi (IOMOU) wenye lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya ukaguzi meli zinazoingia katika bandari za nchi wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Matukio ya picha wakati wa ufungaji wa Mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi (IOMOU) wenye lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya ukaguzi meli zinazoingia katika bandari za nchi wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Matukio katika picha ya pamoja katika makundi mbalimbali mara baada ya kufungwa kwa Mkutano wa 27 wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano ya Ukaguzi wa Meli katika Bahari ya Hindi (IOMOU) wenye lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya ukaguzi meli zinazoingia katika bandari za nchi wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Related Posts