Ayonga ndiye mbabe wa Gymkhana

MCHEZAJI maarufu wa klabu ya Dar es Salaam Gymkhana, Kiki Ayonga ameshinda taji la mashindano ya mwisho wa mwezi ya UAP Insurance.

Ayonga ameibuka kidedea kwa njia ya count back baada ya kufungana kwa mikwaju ya net na 79 na Joseph Placid aliyemaliza katika nafasi ya pili.

“Nimefurahi sana kushinda taji hili la mashindano ya mwisho wa mwezi. Ushindani ulikuwa mkubwa wana na kila mchezaji alikuwa anataka kushinda taji,” alisema Ayonga.

Alisema umahiri wake umempa heshima kubwa katika mshidano hayo yaliyokuwa na ushindani mkubwa na kushirikisha jumla ya wachezaji wengine 86.

“Unapozungumzia ushindani wa kweli, kwa upande wa mashindano ya UAP Insurance, mambo yalikuwa tofauti sana, hata aina ya ushindi wangu unaonyesha jinsi gani ushindani ulikuwa mkali mpaka kufikia hatua ya kurejea kuhesabia mashimo (countback) ili kumpata mshindi, unajona jinsi gani wachezaji wote walivyopania Zaidi ya kwanza,” alisema.

Kwa upande wa Division B, Danstan Kolimba alishinda taji kwa jumla ya mikwaji ya net 70 na kumshinda Chali Said ambaye alimaliza katika nafasi ya pili kwa mikwaju 73.

Katika Division C, Karim Jamal alishinda kwa  mikwaji 74 ya net huku Fahmy Mbarak alishika nafasi ya pili kwa mikwaju 75 ya net.

Kwa upande wa wachezaji wa kike, Jennifer Mbarawa alishinda kwa mikwaju 70 ya net wakati nafasi ya pili ikienda kwa Maryanne Mugo akwa mikwaju 72 ya net.

Kwa upande wa junior, Mikoh Makawago alishinda kwa mikwaju 69 ya net ambapo kwa upande wa wachezaji wageni, Alvin Aguiar alishinda kwa  mikwaju 74 ya net.

Katika mashindano ya kupiga mipira umbali mrefu (Longest Drive, Julius Mwinzani alishinda kwa wanaume na kwa wanawake mshindi alikuwa Jen Mbarawa  wakati kwa upande wa Nearest to Pin Joseph Placid alishinda kwa wanaume na Joyce Ndyetabura alishinda kwa upande wa wanawake.

Mashindano haya yalikuwa sehemu ya michakato endelevu ya kuboresha kiwango cha mchezo wa gofu hapa nchini.

Related Posts