Noela apoteza 90 za kwanza Ulaya

BEKI wa kati wa ASA Tel Aviv inayoshiriki Ligi ya Israel, Mtanzania Noela Luhala amepoteza mchezo wa kwanza akiwa na klabu mpya akitumika kwa dakika zote 90 dhidi ya KG Women Soccer kwa mabao 2-0.

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga Princess inayoshiriki Ligi ya Wanawake nchini ni mara ya kwanza kucheza nje ya mipaka ya Tanzania.

Akiwa Mtanzania pekee kwenye kikosi hicho ambacho siku chache kilimsajili winga wa zamani wa Simba, Mnigeria Olaiya Barakat ambao wote wamecheza kwenye mchezo huo.

Akizungumza na Mwanaspoti Nje ya Bongo, Noela alisema wamecheza mchezo wa nusu fainali ya kwanza na kupoteza kwa mabao 2-0 kwenye michuano ya Israel Women’s Athena CUP.

Alisema wamepoteza mchezo huo wakiwa ugenini akiamini watafanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Septemba 05 utakaowapa nafasi ya kucheza fainali.

“Mchezo ulikuwa mgumu lakini sasa mawazo yetu yapo kwenye mchezo wa marudiano ni mara ya kwanza kucheza Ulaya nikiaminiwa kwa dakika zote 90,” alisema Noela.

Related Posts