Halmashauri lipeni madeni ya wazabuni kuongeza ufanisi katika kazi

Halmashauri ya wilaya ya Geita imeagizwa kulipa madeni wanayodaiwa na wazabuni pamoja na watumishi ili kuwasaidia kuongeza ufanisi katika kazi wanazozifanya kwa manufaa ya Halmashauri ya wilaya hiyo.

Wito huo umetolewa na Katibu tawala wa Wilaya ya Geita Lucy Beda wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo ambacho kilikuwa maalumu kwaajili ya kufunga hesabu za halmashauri ambapo ameeleza kuwa malimbikizo ya madeni yanapunguza ufanisi wa watumishi kufanya kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Karia Rajabu amesema watalifanyia kazi agizo hilo na tayari taarifa ya hesabu za halmashauri hiyo zipo tayari na zitatumwa kwa Mkaguzi wa hesabu za serikali hivi karibuni.

Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Charles Kazungu amewaelekeza madiwani kutoa ushirikiano kwa watumishi wakati wanapopita katika maeneo yao kwaajili ya kukusanya mapato.

Related Posts