HYATT REGENCY YAZINDUA HUDUMA YA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI (BUREAU EXCHANGE)

Hyatt Regency Dar es Salaam, Kilimanjaro imezindua huduma mpya ya kubadilisha fedha za kigeni (Bureau Exchange) kwa lengo la kurahisisha utoaji huduma kwa wageni wanaofika hotelini hapo.

Mbali na hilo pia wanatimiza takwa la kisheria la Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayohitaji bili zote kulipwa kwa fedha za Kitanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo Agosti 30, 2024 Jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Hyatt Regency, Alexander Eversberg alisema kuwa huduma hii itatoa urahisi kwa wageni wa kimataifa na wa ndani kwa kutoa suluhisho la kubadilisha fedha moja kwa moja ndani ya hoteli.

Alisema hapo awali, wageni walilazimika kutembelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya kubadilisha fedha, jambo ambalo lilisababisha ucheleweshaji na usumbufu.

Aidha alisema huduma hiyo mpya ya ndani, wageni sasa wanaweza kushughulikia shughuli zote za kubadilishana fedha kwa urahisi, wakihifadhi muda wa thamani na kuboresha muda wao wa kukaa.

“Kulingana na kanuni za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambazo zinahitaji malipo kufanywa kwa fedha za ndani, Bureau Exchange yetu itarahisisha kubadilisha fedha za kigeni kuwa Shilingi za Kitanzania pekee”. Alisema Eversberg.

Kwa upande wake Afisa Masoko na Uhusiano wa Hoteli ya Hyatty Regency Dar es Salaam, Lilian Mduda alisema kuwa hoteli yao imekuwa ya kwanza kutekeleza sheria mpya ya BoT ili kutatua changamoto za kubadilisha fedha za kigeni kuwa Shilingi za Kitanzania.

“Huduma hii itawasaidia wageni kubadilisha fedha zao na kulipia bili walizotumia kwa urahisi”. Alisema







Related Posts