Majogoro atamani taji Sauzi | Mwanaspoti

KIUNGO Mtanzania anayekipiga Chippa United ya Afrika Kusini, Baraka Majogoro amesema anatamani msimu huu kufanya vizuri na kuisadia timu hiyo kuchukua ubingwa baada ya kuukosa mwaka jana.

Kiungo huyo alisajiliwa na Chippa United Agosti 2023 alipita Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar za Tanzania zote zimeshuka daraja kwa misimu tofauti.

Akizungumza na Mwanaspoti Nje ya Bongo, Majogoro alisema msimu uliopita ulikuwa bora kwa upande wake kwani alifanikiwa kucheza kubwa zaidi upendo alioonyeshwa na mashabiki lakini kwa klabu haikuwa hivyo.

Aliongeza, malengo ya Chippa ilikuwa kuchukua ubingwa ama kumaliza kwenye nafasi tatu za juu badala yake ikamaliza nafasi ya 12 kati ya timu 16.

“Tunapambana kuhakikisha tunapata nafasi na kuendelea kuaminiwa na kocha kwa sasa tupo kwenye maandalizi ya msimu mpya na naamini msimu huu malengo ya kuchukua ubingwa yatatimia kutokana na kujiandaa mapema pamoja na usajili uliofanywa,” alisema Majogoro.

Kiungo huyo amecheza jumla ya mechi 18 za Ligi akitumika kwa dakika 1332 akiwa hajafunga bao lolote.

Ni kama ana kismati cha matokeo mazuri kwani anapocheza dakika nyingi timu hiyo huondoka na ushindi ama sare akionekana ni mchezaji mwenye msaada mkubwa klabuni hapo.

Royal AM (90) 0-0, Golden Arrows  (90) 1-1

Orlando Pirates (77) ilipoteza kwa 2-0, Swallows (46) ikifungwa 2-1, Supersport  (71) ikishinda 2-0, TS Galaxy  (90) ikishinda 2-0, Kaizer Chiefs (46) ikishinda 2-0, Cape       Town Spurs (90) ikishinda 2-0 na Polokwane (46) ikipoteza 1-0.

Mechi nyingine dhidi ya Mamelodi Sundown (45) ikipoteza 2-0, Ravens (56) ikishinda 2-1, Richard Bay (79) ikishinda 3-0, Stellenbosch (56) 1-1, Cape Town City (90) 1-1, Supersport (90) ikishinda 1-0, Richard Bays (90) ikishinda 2-1, Royal AM (90) ikifungwa 3-2 na Cape Town Spurs (90) ikishinda 1-0.

Related Posts