Mashirika binafsi toeni huduma katika halmashauri zote

Serikali Mkoani Geita imeyataka Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto za kiuchumi , kimaendeleo na kiutamaduni sambamba na kulinda Mila na Desturi za Kitanzania.

Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Geita Dkt. Elfasi Msenya katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) 2024 uliotanyika katika ukumbi wa Mkutano EPZ Bombambili Mjini Geita huku akiyaagiza Mashirika yanayotoa huduma ziwe zinawafikia wa wananchi walioko Vijijini.

“Lakini pia lipo changamoto hasa ngazi za utekelezaji kwa Mashirika haya ile miradi tuliyoibua tumeyaweka Jumla mno najua kuna miradi ngazi ya sekta ya elimu , sekta ya Maji , sekta ya kilimo sasa hatuyaainishi kwa sababu tupokwenda kutekeleza kule chini inatubidi kutumia wataalamu walioko kule chini hiyo tunapokuwa na mradi wa Jumla unakuta mradi wa kilimo unatekelezwa na mtaalamu wa Maji , ” Dkt. Msenya.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Viwanda Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Geita Ndg. Charles Chacha ameyapongeza Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali kwa kukutana huku akiayataka Mashirika hayo kuwa mstari wa Mbele katika kupinga vitendo upotoshaji kwenye Jamii.

“Tumeona mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali kwa nchi zingine hata huku kwetu yakijishirikisha masuala ambayo yanapotosha maadili ya Jamii na Hivyo pamoja na kwamba yanalenga kwamba yanasaidia lakini kuna maeneo mengine yanaleta shida , ” Kaimu Katibu Tawala Chacha.

Naye Mwenyekiti wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ndani ya Mkoa wa Geita Bi. Paulina Majogolo ameyataka Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuhakikisha yanafuata sheria, kanuni na Taratibu wakati wa utekelezaji Majukumu yao kama Asasi za Kiraia.

Related Posts