Polisi kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi baada ya mafunzo Marekani.

Kamishna wa Polisi Utawala na Menejimenti ya Rasilimali wa watu CP Suzan Kaganda amesema kuwa baada ya kufunguliwa kwa Mafunzo ya askari wa kike na wasimamizi wa sheria duniani Jeshi la Polisi Nchini Tanzania kuendelea kutoa huduma bora na nzuri kwa wananchi kutokana na mafunzo wanayokwenda kupata.

Ametoa kauli hiyo leo Jiji la Chicago Nchini Marekani mara baada ufunguzi wa mafunzo kwa askari wa kike na wasimamizi wa sheria IAWP ambapo amebainisha kuwa Jeshi Polisi Nchini Tanzania litanufaika mafunzo hayo ambayo yatakuwa na tija katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji wa Jeshi hilo.

Awali Rais wa Shirikisho la askari wakike na wasimamizi wa Sheria Duniani Deborah Friedl akaeleza matumaini yake ni kuona mwaka unaofuata shirikisho hilo linaendelea na kuwa na Nchi na idara nyingi shiriki katika mafunzo hayo huku akibainisha kuwa shirikisho hilo litaendelea kuweka mazingira na ushawishi wa upendeleo kwa askari wa kike duniani IAWP.

Kwa upande wake afisa wa Polisi ambaye ni Mstaafu Bwana John Catanzara anayeshughulika na masuala ya unyanyasaji wa wanawake akaenda mbali na kumpongeza mwanamziki aliyeimba wimbo wakati waufunguzi na wadau wengine ambao wamekuwa chachu ya kumuinua mwanamke na wanawake wasio na sauti huku akiweka wazi kuwa shirika lao litaendelea kushughulikia changamoto zote za wanawake.

 

Related Posts