Rais Samia ateua ma-DC wapya watatu, ahamisha 14

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewateua wakuu wa wilaya wapya watatu, huku wengine 14 akiwahamisha vituo vyao vya kazi.

Uteuzi na uhamisho huo umefanyika leo Jumatatu Septemba 2, 2024.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Septemba 2, 2024 na Kaimu Mkurugenzi  wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu ikinukuu taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mosses Kusiluka, imeeleza Rais Samia amewateua; “Luteni Kanali Fredrick Faustin Komba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Mohamed Mtulyakwaku kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui na Olivanues Paul Thomas kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa.”

-Halima Okash amehamishwa kutoka Wilaya ya Bagamoyo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba.

-Gerald Mongella amehamishwa kutoka Wilaya ya Chemba kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua.

-Dk Rashid Chuachua amehamishwa kutoka Wilaya ya Kaliua kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma.

-Salum Abdallah Kali amehamishwa kutoka Wilaya ya Kigoma kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido.

-Shaibu Ndemanga amehamishwa kutoka Wilaya ya Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.

-Victoria Mwanziva amehamishwa kutoka Wilaya ya Ludewa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi.

-Abdallah Mwaipaya amehamishwa kutoka Wilaya ya Mwanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara.

-Mwanahamisi Athumani Mukunda amehamishwa kutoka Wilaya ya Mtwara kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga.

-Emmanuela Mtatifikolo amehamishwa kutoka Wilaya ya Arumeru kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati.

-Lazaro Twange amehamishwa kutoka Wilaya ya Babati kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

-Amir Mkalipa amehamishwa kutoka Wilaya ya Hai kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

-Dk Khalfan Haule amehamishwa kutoka Wilaya ya Musoma kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya.

-Juma Chikoka amehamishwa kutoka Wilaya ya Rorya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma.

– Zakaria Saili Mwansasu amehamishwa kutoka Wilaya ya Uyui kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe.

Mbali na hao, Rais Samia pia amewateua makatibu tawala wawili, Mohamed Ngasinda kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba, huku Shabani Hamimu ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia.

Katibu Tawala wa Wilaya, Warda Abdallah Obathany amehamishwa kutoka Wilaya ya Iramba kwenda kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni na Stella Msofe amehamishwa kutoka Wilaya ya Kinondoni kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Mick Kiliba kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Kabla ya uteuzi huu, Kiliba alikuwa Ofisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.

Pia Macrice Daniel Mbodo ameteuliwa kuwa Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania (TPC), huku Eliud Betri Sanga akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Related Posts