Mgeni Rasmi ambaye ni Mejeja wa Fedha wa Barrick nchini, Penina Kitundu akimkabidhi cheti cha kuhitimu elimu ya msingi mmoja wa wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya Mwananyamala B, wakati wa mahafali yao hivi karibuni
Meneja wa Fedha wa Barrick nchini Penina Kitundu akizungumza na wanafunzi wakati Mahafali ya
Wanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi Mwananyamala B iliyopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wahitimu wa darasa la saba shule ya Msingi, Mwananyamala B wakiimba kwa furaha wakati wa mahalafali yao hivi karibuni
WANAFUNZI wa darasa la saba wa shule ya msingi Mwananyamala B ya wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wameaswa kuwa waendelee kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao katika maisha yao ya baadaye sambamba na kuweza kukabiliana na mabadiliko mbalimbali yanayoendelea kutokea duniani hususani ya matumizi ya teknolojia za kisasa.
Wito huo umetolewa na Meneja wa fedha wa Barrick nchini, Penina Kituku, ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwakilisha kampuni hiyo ambayo ofisi zake pia ziko jirani na shule hiyo, wakati wa mahafali ya Wanafunzi wa darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo na kuhudhuriwa na viongozi,walimu na wazazi wa wanafunzi.
Akijibu risala ya wanafunzi,Penina amesema changamoto mbalimbali walizotajwa zitafikishwa kwa wahusika zifanyiwe kazi na aliwaasa wanafunzi kuzingatia masomo na kuwa na maadili mema katika safari yao ya elimu ili waweze kutimiza ndoto zao na kuweza kukabiliana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea duniani kwa kuwa wanategemewa kuwa nguvu kazi ya Taifa katika miaka ijayo.
Aidha ametoa pongezi kwa walimu wa shule hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuweza kuleta mafanikio ya wanafunzi kufaulu vizuri katika mitihani ya kitaifa iliyopita na kuifanya shule hiyo kuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika ngazi ya wilaya na mkoa wa Dar es Salaam.Vilevile aliwataka wazazi kushirikiana na walimu wakati wote katika malezi ya watoto ,kuwawezesha na kuwafuatilia ili waweze kupata mafanikio na kuwa raia weka katika siku za mbele.