Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Jumla ya waombaji laki moja elfu ishirini na nne mia mbili Themain na sita (124,286) wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo vikuu themanini na sita (86) vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi katika shahada ya kwanza, na jumla ya programu 856 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 809 mwaka 2023/2024 ikiwa ni ongezeko la programu 47 za masomo.
Katibu Mtendaji Tume ya vyuo vikuu Tanzania Profesa Charles Kihampa ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma katika mkutano na wanahabari.
Amesema katika awamu ya kwanza ya udahili jumla ya waombaji 98,890 sawa na asilimia 79.6 ya waombaji wote walioomba udahili, wamepata udahili kwenye vyuo walivyoomba. na idadi ya waombaji wa udahili na watakaofahiliwa inatarajia kuongezeka katika awamu ya pili ya udahili.
Aidha Prof. Kihampa amesema waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanapaswa kithibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo tarehe 3 hadi Tarehe 21 Septemba 2024, uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia Namba maalum ya siri iliyotumwa wakati wa kuomba udahili.
Hata hivyo Tume inaelekeza vyuo vya elimu ya juu nchini kutangaza programu ambazo bado Zina nafasi na waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili awamu ya pili kama ilivyooneshwa Kwenye kalenda ya udahili iiyoko katika tovuti ya TCU (www.tcy.gi.tz).
Mwisho Prof. Kihampa ametoa wito Kwa waombaji wa udahili wa shahada ya kwanza wanakumbushwa Kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe Moja kwa Moja Kwenye vyuo husika, kwae wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuoe vyote vimeelelezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo ma taratibu zilizowekwa.