AWAMU YA PILI YA UDAHILI WA VYUO VIKUU 2024/25 YAFUNGULIWA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa leo Septemba 03, 2024 ametangaza kukamilika kwa Awamu ya Kwanza na kufunguliwa kwa Awamu ya Pili ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Makao Makuu ya TCU, Jijini Dodoma, Profesa Kihampa amesema kuwa Awamu ya Pili ya Udahili wa Shahada ya Kwanza inaanza leo hadi Septemba 21, 2024.

Aidha, amewaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Kwanza kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.

Kwa wale waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Kwanza ya udahili, Profesa Kihampa amebainisha kuwa wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo tatehe 03 hadi 21, Septemba 2024.

Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanapaswa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.

#KoncepTvUpdates

Inaweza kuwa picha ya Watu 4 na watu wanaosoma
Inaweza kuwa picha ya Watu 11 na watu wanatabasamuInaweza kuwa picha ya Watu 6, chumba cha habari, jukwaa na maandishi

Related Posts