AZAM FC YAFIKIA MAKUBALIANO NA KOCHA YOUSSOUPH DABO KUACHIA NGAZI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC imetangaza kuwa imefikia makubaliano na kocha Youssouph Dabo kuacha kuendelea kufanya kazi na klabu hiyo kuanzia leo, Septemba 3, 2024. Dabo, ambaye aliyehudumu kwenye klabu hii kwa mwaka mmoja, anaondoka pamoja na wasaidizi wake wa benchi la ufundi waliomsaidia wakati wote wa kipindi chake cha kazi.

Azam FC inamshukuru Dabo kwa weledi wake na kujitolea bila kuchoka katika kipindi chote alichokuwa sehemu ya timu hiyo, na inamtakia mafanikio mema katika hatua zake zijazo. Katika kipindi hiki cha mpito, bodi ya klabu itakuwa katika mchakato wa kutafuta kocha mpya, huku programu za timu zikisimamiwa na makocha wa timu za vijana.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts