Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Profesa Hamis Malebo akizungumza katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Tiba ya Mwafrika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Profesa Hamis Malebo akiteta na Mganga Mkuu wa Jeshi wa Kanda Dkt. Lt. Col. Shabhai.
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Profesa Hamis Malebo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuweka
kipaumbele na msukumo kwenye kuendeleza tiba asili nchini.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Profesa Hamis Malebo ameyasema hayo katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika jijini Dar es Salaam.
Amesema Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala ni chombo cha Serikali kilichoundwa Mwaka 2005 chini ya Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na. 23 ya Mwaka 2002, kwa lengo la kusimamia, kudhibiti, kuhamasisha na kuendeleza
huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini.
Maadhimisho hayo kauli mbiu “Kusimamia utoaji wa huduma bora na salama za Tiba Asili kupitia mifumo sahihi ya udhibiti”.
Amesema salamu za
Waganga katika maadhimisho hayo Kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ni Mitano Tena.
Amesema kuwa utafiti wa uwezo wa dawa wameangalia kuwa ni uwepo wa Bajeti finyu kwa NIMR,Utafiti wa usalama na ubora wa dawa asili GCLA, TBS
Vyuo vikuu kwenye Molecules/Viamilifu dawa, preformulation & formulation
Profesa Malebo amesema katika kutimiza majukumu
ya msingi ya Baraza ni wajibu wa kuendeleza mahusiano baina yake na wadau mbalimbali ili kuhakikisha ufanisi wa huduma za tiba asili na tiba Mbadala nchini.
Aidha katika jukumu lingine la Baraza ni kusimamia utoaji wa huduma kwa kuwakumbusha waganga umuhimu wa kuzingatia Sheria, kanuni,
taratibu na miongozo iliyopo, ili kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma bora
na salama.
Aidha amesema Baraza limepata mafanikio makubwa na ya kujivunia
kwa Kusajili wa waganga, dawa na vituo vya kutolea huduma ulianza tangu
mwaka 2010 ambapo kufikia mwezi Juni 2024, jumla ya watalaamu 53,499, Vituo vya kutolea huduma 1,758 na Dawa za asili 127 vimesajiliwa kote nchini na kukabidhiwa leseni za kutoa huduma za Tiba Asili na Tiba
Mbadala.
Hata hivyo amesema udhibiti wa dawa, vituo na matangazo kwa mujibu wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na. 23 ya Mwaka 2002, Ibara ya 8(2) Sehemu 4(3)a hadi h, Baraza limekuwa likitimiza jukumu la kudhibiti dawa za asili kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Wizara iliyowaidhinisha na kukasimu majukumu kwa Mamlaka za TMDA, TBS, Maabara ya Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali, NIMR, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Tiba Asili (MUHAS) kupima dawa asili na kushiriki kama wajumbe wa Kamati ya kusajili dawa asili.
Ametoa rai rai kwa waganga wa tiba asili kusajili dawa
zao. Profesa Malebo amesema Baraza linayo miongozo ya udhibiti wa vituo na matangazo.
Amesema katika kuendeleza tiba asili nchini, Baraza limefanikiwa kupata shamba la ekari 126 lililopo Mkoa wa Pwani Wilaya ya Kisarawe katika Kijiji cha Mzenga B kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Ubora wa Tiba Asili pamoja na shamba darasa la miti dawa.
Profesa Malebo amesema shamba hilo tayari lina Hati ya Kimila na hivyo Baraza linaomba kupewa fedha kwa ajili ya miradi
hiyo ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kupata Hati Milki ya Serikari kwa manufaa endelevu ya tiba asili nchini.
“Baraza linayo furaha kubwa kwa kuwa Wizara ya Afya imeanzisha huduma Jumuishi ya baaadhi ya dawa za asili zilizosajiliwa na Baraza kutumika katika
hospitali za rufaa za Mikoa saba ambayo kwetu ni fursa nchini kwa kukabidhiwa leseni za kutoa huduma za Tiba Asili na Tiba
Mbadala”amesema Profesa Malebo.
Amesema kuhusiana na udhibiti wa dawa, vituo na matangazo, kwa mujibu wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na. 23 ya Mwaka 2002, Ibara ya 8(2) Sehemu 4(3)a hadi h, Baraza limekuwa likitimiza jukumu la kudhibiti dawa za asili kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Wizara iliyowaidhinisha na kukasimu Majukumu mamlaka za TMDA, TBS, Maabara ya Wakala wa Mkemia Mkuu
wa Serikali, NIMR, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Tiba Asili (MUHAS) kupima dawa asili na kushiriki kama wajumbe wa Kamati ya kusajili dawa asili.
Amesema katika mikakati Tiba Asili Serikali iendelee kupanua wigo ili dawa hizo ziweze kutumika katika ngazi zote za vituo vya afya nchini.
Profesa Malebo amesema changamoto zinazolikabili baraza hilo ni udhibiti mdogo wa dawa za asili jambo ambalo linapelekea matumizi
ya dawa zisizo salama au zisizo na ufanisi,Kuwepo na mwamko mdogo katika kusajili dawa asili kutokana na waganga kulalamikia gharama kubwa za upimaji.
Amesema kuna malalamiko ya watengeza dawa za asili wanaopaza sauti kuhusu
utaratibu wa kusimamia dawa asili zinazotumika kwenye Huduma
Jumuishi.
Aliongeza kuwa kuna upungufu wa utafiti na ukosefu wa ushahidi wa kisayansi, kuhusu ufanisi na usalama wa dawa za asili na tiba asili kwa ujumla, jambo
linalopelekea ugumu wa tiba hizi kukubalika na kuunganishwa rasmi
katika mfumo wa afya.
Mzozo wa maslahi kati ya tiba za kisasa na tiba za asili unaweza
kuzuia ushirikiano na maendeleo. “Watalaamu wa tiba za kisasa wanaweza kuona tiba asili kama mshindani badala ya kuwa mwenza au mbadala wa matibabu.
Amesema kuna uelewa mdogo kwa jamii na watalaamu wa afya nchini kuhusu
tiba asili, jambo linalochangia kutokuaminika na kupelekea matumizi
yasiyo sahihi.
Profesa Malebo amesema baadhi ya watalaam wa tiba asili kujihusisha na imani potofu, jambo linalochangia migogoro na matukio ya kikatili katika jamii, hivyo
kushusha hadhi na heshima ya tasinia ya tiba asili.