HOSPITALI YA KAIRUKI YATOA MAFUNZO YA HIFU KWA MADAKTARI BINGWA KUTOKA KENYA

HOSPITALI ya Kairuki imetembelewa na Jumuiya ya Madaktari wa Magonjwa ya wanawake kutoka nchini Kenya , Obstetrical and Gynaecological Society (KOGS) wakiongozwa na Rais wa jumuiya hiyo Dkt. Frederick Kireki.

Ziara hiyo imelenga kufanya utalii tiba ili kuboresha huduma za afya Afrika Mashariki na Duniani kwa ujumla.
Katika ziara hiyo ugeni huo umepata mafunzo juu ya huduma mpya na ya kisasa itolewayo na Kairuki Hospital ya kuondoa uvimbe bila upasuaji kwa kutumia mtambo wa HIFU Pamoja na huduma ya Uzazi Pandikizi inayoptolewa na Kairuki Hospital Green IVF.
Akizungumza katika mkutano huo Kaimu Mkuu Mkurugenzi wa Kairuki Hospital Dkt. Muganyizi Kairuki Amesisitiza juu ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili ikiwemo kufanya utafiti. “Ushirikiano wetu udumishe lakini pia tuwe na Tafiti zetu wenyewe juu ya matibabu tofauti tofauti katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki.”
Kwa upande wake Rais wa Jumuiya hiyo Dkt. Frederick Kireki ameishukuru Kairuki Hospital Pamoja na mapokezi makubwa waliyoyapata ambapo amesisitiza juu ya kauli mbiu ya “MGONJWA KWANZA” kuwa ni jambo la kujifunza.
aidha ugeni huo wa Madaktari wa Magonjwa ya wanawake, ambao upo Kairuki Hospital kwa muda wa siku mbili, umepata nafasi ya kujionea Mubashara namna ambavyo mtambo wa Kuondoa Uvimbe bila kufanyiwa Upasuaji unavyofanya kazi ya kutibu mgonjwa

Related Posts