MBUNGE KOKA ATEMA CHECHE KUWAPIGA JEKI UVCCM MRADI WA KAMPUNI


NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo amepania kuwainua vijana na kuwaondoa katika wimbi la umasikini kwa kuwachangia gharama mbali mbali kwa ajili ya kuanzisha kampuni ya umoja wa vijana wa (UVCCM) Wilaya ya Kibaha mjni ambayo itawasaidia katika kujikwamua kiuchumi.

Koka ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha baraza la UVCCM Wilaya ya Kibaha mjini na kusema kwamba amekubali kwa moyo mmoja kuwaunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na vijana hao ya kutaka kuanzisha kampuni ambayo itakuwa ikijikita zaidi katika shughuli mbali mbali.

Alibainiwa kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaweka mipango madhubuti kwa vijaana hao kuweza kuwa na miradi mbali mbali ya kimaendeleo hivyo atachangia gharama mbali mbali ambazo zitahitajika ikiwemo kufanya usajili wa kampuni hiyo ambayo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa vijana hao.

“Vijana mimi kama mbunge wenu nipo pamoja na nyinyi na Risala yenu nimeisikia ya kutaka kuwa na kampuni ambayo itakuwa ikifanya shughuli mbali mbali kwa hiyo mimi nitachangia gharama mbali mbali ikiwemo kampuni hiyo kupata usajili na nina imani kwamba taratibu zote zikikamilika kampuni hiyo itaanza kufanya kazi kwa maslahi mapana ya vijana wa jimbo la Kibaha mjini,”alisema Koka

Aidha Mbunge huyo aliwataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa kitu kimoja na kuachana kabisa na kuwa na makundi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu kwani lengo ni kuweza kushinda katika mitaa yote 73.

Kadhalika Mbunge Koka amewasihi vijana kufanya kazi zao kwa ushirikiano ikiwa pamoja na kuheshimu viongozi mbali mbali wa chama na serikali walioko madarakani kwa ngazi zote za kiutawala na kutengeneza misingi imara ya kuwa karibu na jamii kwa makundi yote bila ya kuwa na ubaguzi wowote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibaha mjini Ramadhani Kazembe amesema kwamba malengo ambayo wamejiwekea ni kubuni miradi mbali mbali ya kimaendeleoambayo itaweza kuwasaidia vijana kuondokana na umasikini ikiwa pamoja na kujiongezea kipato.

Kazembe alisema kwamba ana imani kubwa kampuni hiyo pindi itakapokamilika itakuwa ni moja ya fursa ya kipekee kwa vijana wa UVCCM kuweza kupata fursa za ajili kutokana na shughuli mbali mbali ambazo zitakuwa zikifanyika na kuwahimiza vijana waweze kuwa na umoja na mshikamano katika kukijenga chama pamoja na jumuiya zake zote.


Related Posts