Mchenga Star yajuta kuikosa UDSM Dar

POINTI 21 zilizofungwa na UDSM Outsiders katika robo ya tatu katika mchezo dhidi ya Mchenga Star ndizo zilizochangia timu hiyo kushinda mchezo huo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL).

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, kocha mkuu wa  Mchenga Star, Mohamed Yusuph  alisema makosa madogo waliyofanya uwanjani ndiyo yaliyochangia kupoteza mchezo huo.

Yusuph alisema wanajutia makosa hayo na kwamba, hilo ni darasa tosha kwao kwa michezo ijayo.

Katika mchezo huo UDSM ilishinda kwa pointi 60-59 katika Uwanja wa Donbosco, OysterBay, ambapo Mchenga Star itabidi ijilaumu kwa kukosa ushindi katika mchezo huo, hasa baada ya kuongoza kwa kipindi kirefu.

Kwenye mchezo Mchenga Star ilianza robo ya kwanza ikiongoza kwa pointi 12-11, 24-14 na hadi kufikia mapumziko ilikuwa mbele kwa pointi 36-25.

Lakini mambo yalibadilika katika robo ya tatu ambapo UDSM Outsiders ilipata pointi 21-10 na 14-13.  

Katika mchezo huo Tyrone Edward wa UDSM Outsiders aliongoza kwa kufunga pointi 21 na kati hizo alifunga katika maeneo ya mitupo mitatu ‘three point’ mara tano

akifuatiwa na Mwalimu Heri aliyefunga pointi 17, huku  upande wa Mchenga Star aliyeongoza alikuwa Jordan Jordan aliyefunga pointi 12.

Related Posts