Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa akiweka Kadi katika Gati Janja kufanya kwa ajili ya kufanya malipo ya usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka uliofanyika katika Kituo Kikuu cha Kimara jijini Dar es Salaam.
*Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani watajwa kufuatwa uwezo wao kuwekeza Mabasi Yaendayo haraka
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Kampuni ya Kutoa Huduma ya Mabasi (UDART) kukaa pamoja katika kufanya suluhisho ya kupatikana kwa Mabasi kufikia Desemba Mwaka huu.
Hayo ameyasema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa wakati akizindua Kadi Janja na Mageti janja kwa ajili ya kununua na kuhakiki tiketi za usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka uliofanyika katika Kituo Kikuu cha Kimara jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa DART na UDART wakikaka pamoja na kutafuta watu wa kuleta Mabasi watapatikana ndani hata bila kutafuta watu wa nje kwani uwezo huo wanao kufanya hivyo.
Hata hivyo amesema Train ya mwendokasi ya Dar es Salaam kwenda Dodoma imepunguza Mabasi ambapo ni fursa ya wafanyabiashara kuwekeza katika mradi wa kusafirisha abiria katika jiji la Dar es Salaam.
Mchengerwa wakati akizindua kadi hizo amepeleleka pongezi kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Kamati ya Bunge kuhusu kuachana na tiketi za Karatasi.
Amesema Kadi Janja na Mageti janja kwa ajili ya kununua na kuhakiki tiketi kwa ajili ya matumizi ya usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka litasaidia kuondoa changamoto ya foleni ya ununuzi wa tiketi vituo vya mwendokasi.
“Nia ya Rais ni kuhakikisha tumeboresha usafiri wa Umma katika Jiji la Dar es Salaam kwa kumaliza changamoto zote za abiria kabla ya kwenda kwenye majiji mengine” Amesema Mchengerwa.
Mchengerwa watumishi wa DART pamoja na watoa huduma wake kuhakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano katika kutoa huduma bora kwa wananchi na kujibu hoja za abiria kwenye Mradi wa DART.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi ya Yaendayo Haraka (DART) Dkt. Athuman Kihamia, amesema kuwa mfumo huo unakwenda kurahishia abiria kusafiri kwa wakati pia matumizi ya Kadi pamoja na mageti janja vitasaidia mradi kati katika utunzaji wa mazingira na kupunguza foleni.
“Mfumo huu uliojengwa na Wataalam wa Mabasi Yaendayo Haraka una faida nyingi ikiwemo kuondoa uchafuzi wa mazingira, zitasaidia kuondoa usumbufu wa chenji pia kuondoa foleni za kununua tiketi, pia kadi hizi zina ubora ukilinganisha na nyingine zinazotumika huko” Amesema Dkt. Kihamia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART, Dkt. Florence Turuka amesema kwa DART ni jambo la fahari kuona mifumo inaimarika kwenye kuendesha usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka na dhamira yao ni kuona kuwa mifumo hii inarahisisha na kuleta tija Jijini Da es Salaam.
Amesema kadi na Mageti janja yaliyozinduliwa yanayotokana na Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji nauli (AFCS) ni juhudi za serikali katika kutumia wataalam wa ndani kuunda mifumo itakayotoa suluhu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika kuzifikia huduma.