TIMU za Risasi na Veta zinatarajia kuchuana Jumamosi ijayo katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Shinyanga mchezo unaopigwa kwenye Uwanja wa Risasi.
Akizungumza na Mwanaspoti kwa simu kutoka Shinyanga, kamishna wa Ufundi na Mashindano Kikapu mkoani humo, George Simba alisema nusu fainali nyingine itachezwa Jumapili kati ya Kahama Sixers na B4 Mwadui.
Alisema mfumo utakaotumika katika nusu fainali hizo ni timu kucheza mara tatu maarufu kama best of three play off.
“Timu itakayoshinda mara mbili mfululizo itaingia fainali,” alisema Simba.