Watu zaidi ya 400 wanyongwa Iran mwaka huu – DW – 03.09.2024

Kwa mujibu wa kundi la wataalumu huru 11 wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, takriban watu 81 waliuawa nchini Iran mwezi Agosti pekee, idadi kubwa zaidi ya 45 walioripotiwa kunyongwa mwezi Julai. 

Wataalamu hao wanaoteuliwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa lakini hawazungumzi kwa niaba ya umoja huo, wamesema wana wasiwasi na ongezeko kubwa la watu kunyongwa nchini Iran.

Kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwa ni pamoja na Amnesty International, Iran huwanyonga watu wengi zaidi kwa mwaka kuliko taifa lingine lolote isipokuwa China.

Soma pia: Amnesty laishutumu Iran kwa kuwanyonga watu 173

Hukumu inakiuka sera ya kimataifa

Maandamano ya kupinga kunyongwa nchini Iran
Wataalamu wanalaani ongezeko la hukumu za kifo kutoka kwa watawala wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.Picha: Ali Khaligh/Middle East Images/IMAGO

Aidha wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na wanahabari maalum wanaoripoti hali ya haki nchini Iran na juu ya hukumu zisizo za kisheria na mauaji ya kiholela, walisema hukumu 41 kati ya hizo mwezi uliopita ni za watu waliopatikana na hatia ya makosa ya dawa za kulevya. Wakati hukumu ya kunyongwa kwa makosa ya dawa za kulevya inakiuka sera ya kimataifa.

Wataalamu hao wamekosoa ongezeko kubwa la hukumu za kunyongwa kwa makosa ya dawa za kulevya nchini Iran tangu 2021, huku zaidi ya hukumu 400 zinazohusiana na dawa za kulevya zikitekelezwa mwaka jana pekee.

Pia wamesema wamepokea ripoti zinazoonyesha kwamba majaribio ya hukumu ya kifo nchini Iran mara nyingi hayafikii dhamana ya mchakato unaostahili.

Aidha kundi hilo la wataalamu lilitolea mfano kisa cha Reza Rasaei, muandamanaji wa Kikurdi, ambaye alinyongwa mnamo Agosti 6 kwa mauaji ya mwanachama wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika tukio ambalo alikuwa ameweka bando linalosomeka maneno yasemayo: “Wanawake, Maisha, Uhuru”.

Soma pia: Amnesty: Zaidi ya waandamanaji 100 wameuwawa Iran

Ambaye alihukumiwa kwa ungamo lililoripotiwa kupatikana baada ya kuteswa, na licha ya washitakiwa wenza kufuta ushahidi wao unaomhusisha na mauaji na ushahidi wa kimahakama kupinga kuhusika kwake.

Wataalamu hao wameelezea wasiwasi kwamba watu wasio na hatia wanaweza kuwa wamenyongwa na wanapendekeza kusitishwa kwa hukumu ya kunyongwa.

 

 

Related Posts