JKT Stars inachapa tu BDL

TIMU ya JKT Stars inaendelea kuonyesha makali katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) baada ya kuifunga  Tausi Royals kwa pointi 70-61.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Donbosco, Oysterbay ulishuhudia JKT Stars ikichomoza na ushindi ulioiongezea matumaini ya kufanya vizuri katika mashindano hayo mwaka huu.

Makali ya timu hiyo yalianza kuonekana ilipozifunga Vijana Queens kwa pointi 73-56 na Jeshi Stars 64-59 katika michezo iliyotangulia.

Katika mchezo wake na Tausi Royals iliongoza katika robo ya kwanza kwa pointi 16-15, 16-9, 17-1, 21-20, huku mastaa waliokuwa mwiba kwa Tausi Royals ni Jesca Ngisaise na Sara Budodi.

Usumbufu wa wachezaji hao ulitokana na ufungaji katika mazingira magumu waliyoyapata pale walipokuwa wamebanwa na walinzi wa Tausi Royals.

Kwenye mchezo huo Jesca aliongoza kwa kufunga pointi 32, kati hizo alifunga katika maeneo ya mitupo mitatu ‘three point’ mara tisa, huku Sara akitupia alama 12.

Kwa upande wa Tausi Royals alikuwa Diana Mwendi aliyefunga pointi 15 akifuatiwa na Amina Kaswa pointi 13.

Related Posts