Lapid atowa wito wa kufikiwa makubaliano ya vita vya Gaza – DW – 04.09.2024

Lapid amesema kumaliza vita vya Gaza ni moja ya vipaumbele vya Israel huku akitoa wito pia wa mabadiliko ya uongozi wa kisiasa, katika taifa hilo la Kiyahudi. Kiongozi huyo wa upinzani amesema vita vya Gaza, vitaendelea iwapo serikali ya sasa inayoongozwa na Benjamin Netanyahu itaendelea kuwepo madarakani. Yair Lapid aliyewahi kuwa waziri Mkuu wa taifa hilo na kiongozi wa chama cha Yesh Atid, amesema serikali ya sasa haitaki amani.

Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zasema vita vya Gaza viishe

Wakati hayo yakiarifiwa Waziri wa usalama wa taifa wa Israel Itamar Ben Gvir, anayetokea chama cha mrengo mkali wa kulia cha Otzma Yehudit, awali alisema anafanya kila awezalo kusitisha mazungumzo yanayoendelea kwa sasa, ambayo sio ya moja kwa moja na kundi la Hamas, kuhusu usitishwaji wa mapigano Gaza.

Ben-Gvir amesema Israel haipaswi kuwa na mazungumzo na wauwaji akimaanisha kundi hilo la kipalestina.

Juma lililopita jeshi la Israel lilitangaza kuipata miili ya mateka sita, hali iliyosababisha simanzi na hasira nchini Israel. Muda mfupi baada ya tangazo hilo, maelfu ya Waisraeli waliandamana mjini Tel Aviv wakimshtumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa kuyumbisha juhudi za Marekani, Misri na Qatar za kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita. Waandamanaji pia walitaka juhudi za haraka zifanywe ili mateka wengine wanaoshikiliwa na Hamas mjini Gaza, waachiwe huru.

Uingereza yasitisha kwa muda usafirishaji silaha Israel

Uingereza | Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer Picha: Benjamin Cremel/AP/picture alliance

Ama kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer alitetea uamuzi wa muda uliochukuliwa na serikali yake wa kuzuwia usafirishaji silaha Israel, kufuatia hofu ya kwamba huenda zikatumika kukiuka sheria ya kibinaadamu.

Kier amesema uamuzi huo kwa aina yoyote haumaanishi kwamba Uingereza imeacha kuiunga mkono Israel na kuamini kwamba taifa hilo lina haki ya kujilinda. Amesema Uingereza imechukua uamuzi huo baada ya Wizara ya kigeni kuangalia upya namna Israel, inavyoendesha vita vyake katika ukanda wa Gaza.

Marekani yaishinikiza Israel kufikia makubaliano na Hamas kumaliza vita Gaza

Israel kupitia waziri wake Mkuu Benjamin Netanyahu imekasirishwa na uamuzi huo na kuuita wa aibu. Msemaji wa Baraza la Usalama wa taifa nchini Marekani John Kirby, amesema Uingereza ilikuwa imeshaifahamisha kuhusu hatua hiyo huku akisisitiza kuwa kila nchi ni lazima iamue kama itaiunga mkono Israel na itafanya hivyo kwa kiwango kipi.     

Israel inaendeleza vita vyake katika Ukanda wa Gaza

Ukanda wa Gaza
Mgogoro wa Mashariki ya kati, hadi sasa watu zaidi ya 40,000 wameuwawa tangu vita hivyo vilipoanza Oktoba 7 mwaka 2023Picha: Mahmoud Issa/REUTERS

Na huku hilo likitokea serikali ya Uswisi imeidhinisha muswada wa kulipiga marufuku kundi la Hamas inayoliona kuwa kundi la kigaidi. Usiwisi imesema mtu yeyote atakayekiuka marufuku hiyo ataadhibiwa kwa kifungo jela au faini.

Chini ya sheria hiyo ambayo kwanza lazima iwasilishwe bungeni, Hamas na makundi mengine yaliyo na uhusiano na kundi hilo yatapigwa marufuku.

Netanyahu asema hatasikia la mtu huku vita vya Gaza vikiendelea kupamba moto

Hayo yanafanyika wakati Israel bado ikiendeleza mapigano mjini Gaza huku zaidi ya watu 40,000 wakiuwawa kufikia sasa.

Israel yazidisha mashambulizi katika ukanda wa Gaza

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

afp/ap/reuters

 

Related Posts