Mafanikio ya Tanzania Sekta ya Bahari yaivuta Comoro

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mafanikio makubwa ya Tanzania katika sekta ya bahari yameivutia nchi ya Comoro kutaka kujifunza masuala mbalimbali kupitia Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), ikiwemo uwezo wa kuwahudumia meli, uongozaji wa vyombo vya majini, na utaalamu wa biashara ya bahari ili kujenga rasilimali watu.

Kauli hiyo ilitolewa Septemba 3, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Masuala ya Bahari la Muungano wa Comoro (ANAM), Mohamed Said Dahalani, wakati wa utiaji saini wa hati ya makubaliano kati ya shirika hilo na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI).

“Mahusiano kati ya nchi hizi mbili ni ya muda mrefu, na asilimia 80 ya biashara yetu hutegemea usafiri wa meli kutoka Tanzania. Tumeona jinsi Tanzania ilivyopiga hatua katika mafunzo ya bahari, na ndiyo sababu tumeamua kuingia kwenye mkataba huu wa makubaliano,” alisema Dahalani.

Related Posts