Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza wakati akifungua Jukwaa la Wahandisi Vijana jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Bernard Kavishe, akitoa maelezo kuhusu Jukwaa la Wahandisi Vijana, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi (katikati), Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi, Zena Said (Watatu kulia), Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, (Watatu Kushoto) na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Jukwaa la Wahandisi Vijana jijini Dar es Salaam.
*Msajili wa Wahandisi aahidi kusimama bega kwa bega na Wahandisi vijana
Na Chalila Kibuda Michuzi,Tv
SERIKALI imesema imesema kuwa katika kuandaa vijana wazawa Wahandisi imeweka mkakati wa fursa za ajira katika miradi mikubwa ya ya kimkakati kushiriki.
Fursa za ajira zinazoonekana kuwa changamoto kwa vijana Serikali imekuja na mpango katika sekta zote ya kuwandaa vijana na kuwalea katika maeoneo yao.
Hayo ameyasema Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi wakati akifungua Jukwaa la Wahandisi Vijana lililoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) Jijini Dar es Salaam.
Jukwaa hilo limekwenda na Kauli mbiu ya “Kuwainua Vijana katika safari yao ya Taaluma na Biashara”
Katambi amesema kutengeneza mazingira wezeshi kwa wahandisi wazawa kutekelekea miradi mikubwa ya maendeleo nchini ili kuwainua kichumi kwa Taifa na Mtu mmoja moja.
Amesema Serikali imeanzisha Sera ya maendeleo ya Vijana, lengo lake ni kutatua changamoto za ajira kwa vijana katika maeneo ya ukuzaji wa taaluma, ujuzi, ubunifu na uvumbuzi, Sera hii ni kuangazia namna ya kuinua wazawa katika maeneo mbalimbali” amesema Katambi.
Aidha amesema kuwa kupitia Sera hiyo wataalamu mbalimbali ikiwemo wahandisi watanufaika kwa kuweza kupata nafasi ya kutekeleza miradi ambayo walikuwa wakishindwa kutekeleza awali kutokana na changamoto za kisera na sheria ambapo hata akikosa na alikuwa na vigezo anatoa taarifa katika kupata haki yake aliomba.
Naibu Waziri huyo amesema katika kuhakikisha Serikali inalinda soko lake la ndani pia inadhibiti uagizwaji wa vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi ambavyo vinaweza kupatikana nchini.
Hata hivyo amesema kutokana na vyuo kuzalisha kila mwaka ni bora vijana kuwajibika na kujituma zaidi ambapo wanaweza katengeneza Kampuni zao hata nje ya nchi.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde amesema kuwa Wizara itaendelea kuunga mkono jitihada zinzofanywa na ERB za kuinua Wahandisi ili kuwawezesha kutekeleza miradi mikubwa nchini na kuinuka katika uchumi.
“Niwapongeze kwa kuanzisha jambo hili ambalo litaota, kumea, kukua na kuleta maendeleo kupitia wahandisi hawa, niwahakikishie kuwa Wizara inaandaa mpango kabambe wa kuongea na wadau kuhakikisha fedha nyingi zinapatikana ili kuwasaidia wahandisi kuanzisha Kampuni zao”, ameeleza Dkt. Msonde.
Dkt. Msonde amewataka Wahandisi hao kutumia Jukwaa hilo vizuri ili kuweza kuleta matokeo chanya na hatimaye kuboresha maisha yao na uchumi wa Taifa kwa ujumla kupitia tasnia ya Uhandisi.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi, Mwanasheria Menye Manga amesema kuwa Jukwaa hilo ambalo limeanza mwaka huu linatoa fursa kwa vijana hao kupata ujuzi, uzoefu na maoni kutoka kwa wadau wa Taaluma ya Uhandisi ndani na nje ya nchi.
Ameongeza kuwa jumla ya Wahandisi 24 wamekula kiapo katika Kongamano hilo, na Wanafunzi 15 kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali nchini waliofanya vizuri katika masomo ya uhandisi wamepewa vyeti.
Kwa upande wa Msajili wa ERB, Mhandisi Bernard Kavishe amesema kuwa Kongamano hilo linaenda sambamba na Siku ya Wahandisi pamoja na mbio za riadha maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia programu ya kufadhili walimu wa kujitolea wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa Shule za Sekondari.
Kongamano hili la siku mbili limehudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo wahandisi mbalimbali kutoka ndani ya nchi na nchi jirani za Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini, wadau mbalimbali pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao ya kihandisi kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali nchini.