WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WA JIMBO LA SAME MASHARIKI WAWASILI DODOMA KWA MWALIKO WA MBUNGE

NA WILLIUM PAUL, DODOMA.

WALIMU Wakuu wa shule za sekondari na Wasaidizi wao(Makamu) kutoka katika jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro wamewasili jijini Dodoma kwa mwaliko kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo, Anne Kilango Malecela wa kuhudhuria kikao cha Bunge hapo kesho kujifunza jinsi shughuli zake zinavyoendeshwa.

Walimu hao ambao walipokelewa na mwenyeji wao, Mbunge Anne nyumbani kwake ambapo kesho wanatarajiwa kushiriki katika kikao cha Bunge na badae kukutana na Waziri wa Tamisemi na jopo kutoka Wizara ya Tamisemi na Wizara ya Elimu kubadilishana mawazo ambapo watapata fursa ya kueleza yale waliyonayo kwa viongozi hao.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake, MMkuu wa shule ya sekondari ya Lugulu, Nduga Makenji alisema kuwa, mwaliko huo wa Mbunge Anne utaleta chachu kubwa ya walimu kutimiza wajibu wao pamoja na kuongeza ushirikiano na mshikamano baina ya walimu na Mbunge huyo.

Mwaliko wa walimu hao ni wa kihistoria kwa kada hiyo kualikwa kushiriki katika kikao cha Bunge ambapo zimepita siku chache tangu Viongozi wa Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi Kata ambao ni Mwenyeviti, Makatibu na Makatibu hamasa nao kualikwa kushiriki Bungeni kujifunza jinsi shughuli za Bunge zinavyoendeshwa na badae kupata semina ya kuelekea uchaguzi mkuu.






Related Posts