Abiria mlevi ataka kujifanya rubani angani,ndege yalazimika kutua kwa dharura

Ndege ya easyJet kutoka shirika la ndege la uingereza, iliyokuwa ikielekea kwenye kisiwa cha Kos,nchini Ugiriki, ililazimika kutua kwa dharura Jumanne baada ya abiria mlevi kutaka kujifanya rubani angani.

Tukio hilo lilitokea wakati ndege ilipokuwa angani kwenye urefu wa futi 30,000. Abiria huyo, ambaye alijaribu kufungua milango ya dharura na kupigana na wahudumu, aliharibu mawasiliano ya ndani ya ndege akisema kuwa alitaka kuchukua usukani. Kwa mujibu wa The Sun, mlevi huyo alijaribu kufungua milango ya dharura ili kutoka katikati ya anga.

Wahudumu wa ndege na abiria walifanikiwa kumzuia mlevi huyo na kumshikilia kwa nguvu. Alikamatwa mara baada ya ndege kutua na picha zilionyesha akiwa amelala chini kwenye uwanja wa ndege. Tukio hilo lilitokea kwenye ndege ya Airbus A320 baada ya kukumbwa na mtetemo wa ndege, ambapo mlevi alijaribu kupigana na wahudumu na kutukana rubani akisema atachukua usukani wa ndege. Abiria walishuhudia kwa hofu jinsi alivyokuwa akivuruga hali ndani ya ndege.

Wahudumu walimshikilia mlevi huyo chini ya ndege huku abiria wakipiga kelele na kumzomea. Ndege ililazimika kutua Munich, Ujerumani, ambapo polisi walimsubiri mlevi huyo. Alikamatwa na kufungwa pingu. Abiria walilazimika kutumia usiku wao katika hoteli za eneo hilo na walikuwa wakisubiri ndege nyingine kuelekea Ugiriki.

Aidha EasyJet ilitoa tamko ikisema, “Ingawa matukio kama haya ni nadra, hatuvumilii tabia ya matusi au vitisho.”

Related Posts