DKT. BITEKO ATOA SOMO UZALISHAJI, MATUMIZI YA NISHATI AFRIKA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akihutubia Mkutano wa Hydrogen Barani Afrika unaoendelea Mjini Windhoek, Namibia.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Washiriki wa Mkutano wa Hydrogen Barani Afrika unaoendelea Mjini Windhoek, Namibia. Mkutano huo unakwenda pamoja na maonesho ya teknolojia
mbalimbali zinazotumika katika kuzalisha Hydrogen.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisikiliza kwa makini
maelezo kutoka kwa mmoja wa Washiriki (hayuko pichani) wa Mkutano wa Hydrogen Barani Afrika unaoendelea Mjini Windhoek, Namibia. Mkutano huo unakwenda pamoja na maonesho ya teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kuzalisha Hydrogen.

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri na Waziri wa Nishati, Mhe.
Dkt. Doto Biteko amezitaka nchi za Afrika kubuni na kutumia rasilimali na vyanzo mbalimbali vya nishati vilivyopo kuchochea maendeleo ya uchumi miongoni mwa nchi hizo.

DKt. Biteko amesema hayo (05/09/2024) Mjini Windhoek, Namibia wakati akihutubia Mkutano wa kimataifa kuhusu matumizi ya Hydrogen kwa ajili ya kuzalisha nishati ya
umeme.

Amesema nchi hizo zinahitaji kuunganisha nguvu na kuweka mifumo na sera za kuwezesha matumizi ya teknolojia na mbadala kwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu miongoni mwa nchi washiriki.

Akitoa mfano wa Tanzania, Dkt. Biteko ameueleza Mkutano huo kuwa Tanzania iko katika utekelezaji mkakati wa upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa gharama nafuu na hivyo kuchochea maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla.

Amezitaka nchi hizo za Afrika kuifanya ajenda ya nishati safi kuwa ya pamoja miongoni mwa nchi hizo ambayo inapunguza gharama za uedeshaji na kupungguza
changamoto za kiafya.

Amesema pamoja na changamoto za kifedha, miundombinu na masoko katika matumizi ya Hydrogen, lakini ushirikiano na uhusiano mzuri miongoni mwa nchi za Afrika linaweza kuwa suluhisho.

Amesema Tanzania kwa upande wake itaendelea kuwa kinara katika matumizi ya Nishati safi kwa kushirikiana na mataifa mengine ya Afrika katika kupitia mifumo, miundo sera na sheria zinazolenga katika maendeleo endelevu.

Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah ambaye amewataka washiriki kutumia fursa ya mkutano huo kuanisha mbinu na mkakati unaoweza kutumika kuleta maendeleo ya nchi husika kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Amesema Namibia inajivunia matumizi ya Hydrogen kwa matumizi ya viwanda kwa manufaa nchi hiyo, nchi Jirani pamoja na mataifa mengine yaliyo katika mlengo wa
matumizi ya nishati hiyo.

Tanzania iko katika hatua za awali katika kuendeleza matumzi ya Hydrogen hivyo inatumia fursa ya Mkutano huo kujifunza kuhusu fursa na Changamoto zinazoweza
kujitokeza.

Nchi za Afrika ambazo ziko katika matumizi ya Hydrogen ni pamoja na Namibia, Afrika Kusini, Kenya, Maouritania na Morocco.

Related Posts