CHINA YASITISHA UASILI WA WATOTO KWA NCHI ZA KIGENI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Serikali ya China imetangaza kusitisha rasmi uwasili wa watoto wake na nchi za kigeni, isipokuwa kwa ndugu wa damu au mtoto wa kambo. Hatua hii inakomesha miongo kadhaa ya wageni, hususan familia za Kimarekani, ambao walikuwa wakitembelea China kwa ajili ya kuasili watoto.

Tangazo hili limetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China, ingawa haikutoa ufafanuzi wa kina juu ya sababu za uamuzi huo. Kwa miaka mingi, China imekuwa moja ya nchi kuu kwa uwasili wa watoto, ambapo maelfu ya familia za kigeni, hasa kutoka Marekani, zimepata watoto kupitia mchakato huo.

Mamia ya familia za Kimarekani bado zinatarajia kupata watoto kupitia uwasili nchini humo, lakini hatua hii mpya inatarajiwa kuathiri mipango yao na kubadili mtiririko wa uwasili wa kimataifa kutoka China.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts