CPA. Makalla ataka wafugaji Longido wajitenge na fitna za wanasiasa

Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wake wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA. Amos Makalla ameitoa hofu Jamii ya Wafugaji kwamba Serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye maeneo yao, huku akitaka Ijitenge na Fitna zinazosambazwa na Wanasiasa.

CPA. Makalla ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Jamii hiyo akiwa katika Kata ya Mundarara iliyopo Wilayani Longido mkoani Arusha.

“Fitna hizi naomba mzipuuze, naomba muwe na imani na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Naomba Muwe na Imani na Serikali ya CCM, kwa Sababu Fitna hizi zinasambazwa na Watu ambao Sio wafugaji, Fitna hizi zinasambazwa na Watu ambao Makazi yao ni nje ya Longido wanaishi Mjini na Sio hapa, Endeleeni kuamini Kauli ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan” amesema CPA. Makalla.

Related Posts