MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFUNGUA MASHINDANO YA MAJESHI MOROGORO

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amefungua mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Akizungumza kwenye ufunguzi huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amewataka wanachezo kutumi michezo katika kujipatia kipato na kuliwakirisha vyema Taifa katika mashindano ya Kimataifa.

Pia amesema michezo ni moja ya yenzo muhimu ya kudumisha na kuimarisha mashirikiano mahala pakazi na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wao.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la wananchi Tanzania ( JWTZ) Luteni General Salum Haji Othuman amesema lengo la michezo hiyo ni kuinua vipaji vilivyopo kwenye majeshi nchini na kujiandaa kwajili ya michezo ya kimataifa inayofanyika kila mwaka.

Brigedia Jenerali Said Hamis Said ni Mwenyekiti wa baraza hilo, amesema michezo hiyo imeaanza kutimua vumbi rasmi leo Septemba 6,2024 na yanatarajiwa kufikia mwisho Septemba 15 ambapo mgeni ramsi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Michezo ya majeshi inaundwa na kanda nane ambazo ni Ngome iliyopo chini ya JWTZ na kanda nyingine ni polisi , magereza , uhamiaji , zimamoto na uokoaji , Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kanda ya Idara Maalumu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Michezo itakayochezwa ni soka, netiboli, basketi kwa wanaume na wanawake, volleyball riadha wanaume na wanawake zikiwemo za mbio za kilometa 21.

Mingine ni mpira wa mikono, mirusho ,vishale (Darts) na mchezo wa shabaha kwa kutumia silaha za moto ambayo itafanyika kwenye viwanja vya wazi isipokuwa wa shabaha ambao utatumika katika viwanja maalumu vilivyoandaliwa kutumia silaha hizo.

Related Posts