MAMA NA MWANAYE WAFARIKI BAADA YA KULAWITIWA DODOMA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Mama mwenye umri wa miaka 33, Mwavita Mwakibasi, na binti yake wa miaka 11, Salma Silvesta, wote wakazi wa Mtaa wa Muungano, Kata ya Mkonze, Jijini Dodoma, wamefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa ukatili na watu wasiojulikana.

Tukio hili la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia Ijumaa, Septemba 6, 2024, ambapo inadaiwa walichomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni na mgongoni. Aidha, walifanyiwa ukatili wa kuingiliwa kinyume na maumbile.

Mtoto mkubwa wa marehemu, ambaye jina lake limehifadhiwa, amesema aliamshwa na mdogo wake aliyemwambia kuwa mama yao alikuwa akivuja damu. Mara moja aliamua kumpigia simu bibi yake ili kuomba msaada.

Hadi sasa, polisi wa Mkoa wa Dodoma bado wanaendelea kuchunguza tukio hilo, huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, George Katabazi, akithibitisha kuwa atatoa taarifa zaidi mara atakapomaliza kikao chake.

Wananchi wa eneo hilo wamepokea tukio hilo kwa mshtuko mkubwa, huku wakiomba hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya waliohusika.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts