MONGELLA APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM 2020-2024 KUTOKA KWA RC SHINYANGA

Naibu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kuwasili mkoani hapo kwa ziara ya chama ya siku saba leo, tarehe 6 Septemba 2024. Mongella ni mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Pamoja na kutia saini kitabu cha wageni, Ndugu Mongella pia amepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama 2020-2024 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa.






Related Posts