MWAMBA KUOA PACHA WASIOTAKA KUTENGANA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Mtangazaji wa redio ya kijamii ya Wambaz ya nchini Kenya, Oleman Learat, mwenye umri wa miaka 26, amepanga kukimbia ukapera kwa kuoa wasichana pacha.

 

 

 

 

 

Pacha hao, Anne Samken na Emily Salaon (miaka 20), wameamua kuolewa wote na kijana huyo wakisema hawawezi kutenganishwa, kwa hivyo, wamekubaliana kwamba ni afadhali waolewe na mume mmoja.

 

 

 

 

“Nimeiambia familia yangu kuhusu nia yangu ya kuwaoa hawa pacha haijakataa lakini wanauliza maswali mengi,” Oleman ameliambia gazeti la Taifa Leo na kuongeza kwamba yeye anaona kama anaoa ‘msichana mmoja’ tu kwani wanafanana kwa kila kitu! Japo Oleman anasema atawajengea kila mmoja nyumba yake katika boma moja, pacha hao ambao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha KCA cha jijini Nairobi wamesema itakuwa vigumu wao kukaa mbalimbali.

 

 

 

 

“Sisi hatujawahi kutenganishwa tangu tukiwa shule ya chekechea,” anaeleza Emily. “Walimu walitutenganisha kwa mwaka mmoja tukiwa shule ya Sekondari mwaka wa 2021 (wakiamini ndio tutafanya vizuri katika masomo) lakini tuloishi kwa huzuni na upweke sana.”

 

 

 

 

Oleman anasema alianza uhusiano na warembo hao mwaka jana 2023 na kwamba mwanzo ilikuwa ngumu kuwatofautisha lakini sasa anaweza kuwatofautisha, hasa kwa namna wanavyoongea. Mwanahabari Oleman amesema alikutana kwa mara ya kwanza na pacha hao katika hafla za burudani na kuvutiwa nao.

 

 

 

 

 

“Niliona wanafanana kwa kila kitu. Ukiuliza swali, wanajibu pamoja. Nikaanza kuwachumbia na wakanipenda. Kimsingi huwezi kuongea na mmoja akamtenga mwenzake. Kwa hiyo hata nikipiga simu, lazima niwajumuishe wote wawili,” amesema.

 

 

 

Chanzo: Taifa Leo

Related Posts