Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amefanya ziara fupi ya kujionea hali ilivyo katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiwa ni muendelezo wa mafanikio makubwa Hifadhi hiyo inaendelea kuyapata baada ya filamu ya The Royal Tour iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na uwepo wa treni ya umeme inayopita Mkoani Morogoro
Akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amepata wasaa wa kujionea hali ilivyo katika mbuga hiyo ambapo wageni wameendelea kumiminika na kuongeza mapato ya Hifadhi hiyo na Taifa kwa ujumla
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyo Mkoani Morogoro imepata neema ya kuongezeka kwa watalii kutokana na filamu ya The Royal Tour iliyoasisiwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na uwepo wa treni ya umeme ambayo imerahisisha usafiri wa kufika katika hifadhi hiyo