MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AAPISHWA KUWA KAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA, AAHIDI USHIRIKIANO

Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Prof. Ibrahim Hamis Juma Kushoto akimuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Hamza Johari kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Septemba 07, 2024 jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali ni mtu muhimu sana sio tu kwa mahakama bali Bunge na serikali na pengine ndio maana hula viapo vitatu ikionesha umuhimu wa nafasi yake.

Hayo yamesemwa leo Septemba 07, 2024 na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma wakati wa kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari kuwa Kamishna n mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Amesema kuwa ndio maana anakula viapo vitatu, ambapo ni viongozi wachache sana wanakula viapo vingi zaidi kuliko wengine.

“Hii inaonesha umuhimu wa nafasi yake kutokana na kuwa mtetezi mkuu wa Mahakama mara nyingi watu huwa hawauoni umuhimu wake ….” 

Prof. Juma amesema kuwa kama kunatokea mkwaruzano wowote na kiongozi wa muhimili mwingine au akivuka anga na kuingia kwenye anga la Mahakama kwa kutokujua amesema wananjia nyingi za mashauriano kwa kutumia Mwanasheria mkuu wa Serikali kufikisha ujumbe na kuelimishana kwamba hayo simajukumu yake ni majukumu ya watu wengine kwa kufanya hivyo kumesaidia.

“Aliyevuka anga akielimishwa anashukuru sana anasema nilikuwa sijui kwamba hii anga nilikuwa sitakiwi kufika. Hizo ndio kazi kuu kwani anakuwa mtetezi wa mahakama na ametusaidia sana.”

Pia Prof. Juma amemuasa ahakikishe anafahamu kila kitu kinachoendelea ndani ya mihimili ya serikali lakini pia twatatoa ushirikiano kwenye kila kitu muhimu, kama kuna nyaraka muhimu zimetoka, sera   ni muhimu aelewe, kwani hajui taarifa zitaenda kutumika wapi.

Kwa upande wa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na aliyekuwa  Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Dkt. Eliezer Feleshi, amesema kuwa wana matumaini makubwa na Mwanasheria huyo katika usimaizi wa sheria. 

“Nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ni nafasi ya pekee, anaiwezesha tume kuwa na afisa ambaye kwa dhamana yake anaingia akiwa na uwakilishi kwenye mihimili mingine ya serikali, yeye yupo serikalini anaingia kwenye mabaraza mengi na anaelewa nini kinaendelea Serikalini lakini pia anapoingia bungeni anahakikisha hakuna Matope. 

Pia asema kuwa atampa ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi kwa ufanisi na  kumwezesha kufanya kazi kwa umahiri zaidi.

 Kwa upande wa  Mwanasheria mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa anatambua kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni daraja katika mihimili mitatu ya serikali.

Pia amesema atajitajidi kufanya kazi kwa pamoja, na kuhakikisha kwamba malengo ambayo watajiwekea watayatimiza.

“Nilazima sasa kama Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali tuhakikishe kwamba tunatekeleza majukumu yetu ipasavyo na ule ushiriki wetu katika maeneo yote yanayohitaji mchango tutafanya hivyo kwa weledi lakini pia kwaharaka kutoa huduma ambazo ni bora na zenye tija kwa Taifa letu.” Amesema Johari

Related Posts