Wakati michezo ya majeshi ikiendelea katika viwanja mbalimbali ndani ya Manispaa ya Morogoro, timu ya Polisi ya wanawake imeibuka na ushindi wa point 61 -58 dhidi ya timu ya wanawake ya Magereza.
Mchezo huo umechezwa jioni ya Septemba 7 katika uwanja wa Bwalo la umwema.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, kocha wa Polisi, Nasri Malundila amesema kuwa udhindi huo umetokana na mipango na mikakati waliyoweka pamoja mazoezini.
“Ushindi wetu umetokana na uzoefu wetu kuwa mkubwa na leo hatukutumia nguvu kubwa kwa sababu tunajua bado zipo mechi nyingi mbele yetu, ambapo tunakwenda kukutana na timu zenye uwezo ukubwa,” amesema Malundila.
Naye kocha wa Magereza wanawake, Joseph Matle ametaja sababu ya kushindwa ni kutokana na kutoshiriki katika michezo hiyo kwa miaka mitatu iliyopita ambapo mwaka huu timu hiyo ndio imerejea.
“Hii timu ya Polisi imekuwa na mashindano ya kila mara na hivyo wamekuwa na muda mzuri wa kujiandaa hata hivyo tunakwenda kujipanda Kwa mechi zijazo Ili tuweze kupata ushindi,” amesema Matle.
Ameongeza, “katika mchezo wa Leo sekunde 56 za mwisho tulipata mipira miwili ambayo hatukutumia vizuri.”
Michezo mingine iliyochezwa katika viwanja hivyo ni pamoja na timu ya mpira wa pete wanawake Uhamiaji kuibuka na ushindi wa mabao 72-26 dhidi ya Uhamiaji.